Home Kitaifa SWEDEN KUSHIRIKIANA NA TRA KUONGEZA UWEKEZAJI

SWEDEN KUSHIRIKIANA NA TRA KUONGEZA UWEKEZAJI

Balozi wa Sweden Nchini Tanzania Mhe.Charlotta Ozaki Macias amesema Nchi hiyo itaendelea kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kuchochea Uwekezaji nchini.

Akizungumza wakati alipotembelea Ofisi za TRA makao makuu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 15.01.2025 na kukutana na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda, Balozi Macias amesema TRA imekuwa ikiweka Mazingira mazuri ya Kodi ili kuvutia wawekezaji.

Balozi Macias aliyeambatana na uongozi wa kampuni ya Scania, ameishukuru na kuipongeza TRA kwa kuendelea kuwasikiliza wawekezaji na kutatua changamoto zao za kikodi kwa wakati.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Yusuph Juma Mwenda ameahidi kuendelea kushirikiana na wawekezaji kutoka ndani na nje ya Nchi ikiwemo Sweden na kutatua changamoto zao za kikodi ili kuweka mazingira mazuri ya Uwekezaji na kuwezesha kulipa Kodi kwa hiari.

Kamishna Mkuu Mwenda amesema TRA imekuwa ikijitahidi kuweka mazingira ya usawa katika kukusanya Kodi na kutomuonea mtu yeyote maana Kodi inayokusanywa ndiyo inayotegemewa kuleta maendeleo nchini.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!