MBUNIFU wa Mavazi nchi ya Tanzania mwenye asili ya kitariano Guia martinotti amesema ataendelea kufanya kazi za kibunifu nchini Tanzania kutokana na tasnia hiyo kupewa kipaumbele na wabunifu wengi waliopo nchini humo.
Martinotti ameeleza kwa namna miaka 05 ameishi nchini Tanzania na kupokelewa na Mbunifu na mdau wa tasnia ya mitindo Deogratius kithama kwenye Tamasha lake la mavazi nchini (Tanzania fashion festival) na kuona mwangaza wa kuendelea kunyanyua kipaji chake kushiriki Matamasha makubwa ikiwemo swahili fashion week.
“Watanzania wamekuwa nami bega kwa bega katika kuhakikisha napata nafasi ya kuonyesha bunifu zangu nchi Tanzania akiwemo mdau wa tasnia ya ubunifu na mitindo Deogratius kithama kwenye jukwaa lake pamoja na Mustafa Hassanali ambapo natarajia kushiriki jukwaa hilo Disemba 02 mwaka huu kwa mara ya kwanza.”
Hata hivyo amepongeza Muandaaji wa ‘swahili fashion week ‘ Mustafa Hassanali kwa kuwapa nafasi wabunifu chipukizi kuonyesha bunifu zao pamoja na nchi zingine ambazo zinazungumza lugha ya Kiswahili kushiriki jukwaa hilo kwani inasaidia sana kubadilishana uzoefu baina ya wabunifu chipukizi na wakongwe pamoja na nchi na nchi .
Pia ameeleza shahuku yake kumvalisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu nguo ambayo itaendana na utamaduni wa kiafrika yenye mchanganyiko wa kitenge, khanga pamoja na shuka la kamasai ili iweze kujitangaza Kimataifa nguo hiyo inayoitambulisha kwa namna moja au nyingine nchi ya Tanzania.
“Nigetamani kufanya bunifu ambayo angeweza kuvaa Rais wetu mpendwa na mchapakazi Mama Samia kutokana ni kiongozi ambae amekuwa mchapakazi na amefungua milango mingi ya fursa nchi Tanzania pamoja na kuhakikisha anaiwakilisha na kutambulisha nchi ya Tanzania na vivutio yake hivyo kazi yetu wabunifu kuhakikisha tunatengeneza nguo zenye kuendelea kuitangaza nchi hii kwa mavazi mazuri yenye muonekano wa malighafi ya kitenge na khanga kutoka viwanda vilivyopo nchini humu
..Mwisho.