Home Kitaifa STAMICO YAJA NA SULUHISHO LA MATUMIZI YA MKAA MBADALA UNAOZALISHWA NA MAKAA...

STAMICO YAJA NA SULUHISHO LA MATUMIZI YA MKAA MBADALA UNAOZALISHWA NA MAKAA YA MAWE

Na Magrethy Katengu

Shirika la Madini Taifa (STAMICO) limesema litahakikisha linaongeza juhudi kukabiliana changamoto ya mabadiliko ya Tabia nchi inayosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya matumizi ya mkaa ambao hali hiyo kadri miaka inavyozidi kusongea uoto wa asili umekuwa ikipotea.

Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la madini la Taifa (STAMICO ) Dkt. Venance Mwasse amesema Shirika hilo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1972 na limepitia misukosuko mingi lakini limeendelea kujiendesha na kwa kufanya shughuli zake mbalimbali ikiwemo kufanya tafiti zinazokwenda kuleta suluhisho ya changamoto inayoikabili Jamii ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi inayopelekea uhaba wa mvua ( ukame).

Nchi yetu kadri miaka inavyozidi kusogea nayo inakumbana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi hali hii inasababishwa shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji miti kwa matumizi hasa uchomaji mkaaa hivyo STAMICO tumekuja na suluhisho la kubuni mkaa mbadala ujilikanao kwa jina Rafiki BRIQUETTES ubunifu makini suluhisho la nishati mbadala wa utunzaji mazingira ambapo kuna mitambo ya kutengeneza bidhaa hiyo” amesema Dkt Venance

Mkurugenzi Venance amesema Shirika hilo katika kipindi cha miaka hamsini lilifanya utafiti huo kwa kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo COSTECH,TIRDO,na Vyuo Vikuu hivi karibuni Mkaa abadala uitwa (Rafiki BRIQUETTES ) ubunifu huo makini suluhisho nishati mbadala ya utunzaji mazingira ambapo tayari utafiti huo ulishakamilika na mtambo wa uzalishaji bidhaa na hiyo majaribio yalifanyika STAMICO ikapatiwa cheti na Shirika la viwango Tanzania (TBS) .

Dkt Venance amesema bidhaa iliyozalishwa iko salama kwa matumizi hivyo amewaasa wananchi waachane na kuharibu mazingira kwa kukata uoto wa asili waanze kutumia bidhaa hiyo kwani nayokwenda kuzinduliwa hivi karibuni.

Hata hivyo amesema ubunifu huo wa mkaa mbadala ni mradi mkubwa unakwenda kuleta suluhisho la mabadiko ya tabia nchi na utafiti huo ulianza 2018 na ulifanyika katika hatua mbalimbali ambapo 2019 matokeo yalionyesha mkaa huo ungenza kutumikia mtumiaji angetakiwa kutumia sufuria mpya na jiko lisingefaa tena huku sufuria ikiharibika yote hivyo wakaona haifai matokeo hayo yanakwenda kuongeza changamoto ya gharama na isingekuwa rafiki kwa watu wenye kipato cha chini ikalazimu kurudi maabara Hadi bidhaa hiyo ilipofaa

Hata hivyo utengenezaji wa Mkaa huo mbadala wanatumia mabaki ya makaa ya mawe kwa kuchanganya na maranda ya mbao ambapo uzalishaji huo utafanyika katika maeneo ambayo makaa hayo yanapatikana.

Aidha STAMICO wanatarajia kuiadhimisha miaka hamsini ya Shirika hilo tangu kuanzishwa kwake 1972 na itaafanyika kuanzia Agosti 1-12 mwaka huu kunafaisha hadi kufikia mwaka huu huku kauli mbiu ikiwa “STAMICO na mazingira”” kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo kupanda elfu kumi Dodoma- Ipagala na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na kugawa misaada kwa wagonjwa wanaogua Saratani,kugawa Vifaa Kwa watu wenye uziwi watu wote wanakaribishwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!