Home Kitaifa SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF

SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA NSSF

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Masha Mshomba, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), baada ya kuhitimisha Bunge Jijini Dodoma, Juni 28, 2024.

Mazungumzo hayo yalihusu utaratibu wa ulipaji mafao ambao NSSF imeendelea kuuboresha kupitia mifumo ya TEHAMA. Aidha, Mshomba ameelezea maandalizi ya ulipaji mafao kwa kuzingatia maboresho ya kanuni ya kikokotoo, na ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kujali maslahi ya Watanzania.

Pamoja na hayo, Mshomba alitumia fursa hiyo kumpongeza Dk. Tulia Ackson kwa kuhitimisha Bunge la Bajeti kwa mafanikio makubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!