Akizungumza katika Mdaharo Siku ya Familia Duniani wilayani hapo tarehe 15 Mei 2023, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Ukerewe SP EG. MATIKU alieleza kuwa Katika kujenga familia imara, Baba na Mama wanao wajibu wa kujenga mshikamano imara kwani kila mmoja anao wajibu wa kutimiza Kwa mjibu wa Mila, Kanuni, Sheria na Tamaduni za waafrika.
“…kumekuwa na tabia wanaume (Baba) wanawatelekeza wake zao kwa visingizio vya utafutaji hasa wale wanaojihusisha na masuala ya Uvuvi katika visiwa vya Ukerewe, suala hili ni kosa kwani tunawabebesha wanawake majukumu mazito ya kuihudumia familia, hali ambayo inapelekea vijana (watoto) wengi kuzagaa mtaani kwa kukosa malezi bora ambapo hupelekea watoto hao kujiunga na makundi yasiyofaa kama vile Unyang’anyi, Upolaji, Wizi, Udokozi, Ombaomba Mtaani, Ushoga na Utumiaji wa Madawa ya Kulevya, kila viongozi wa familia (Baba) wawajibike ipasavyo kuhakikisha watoto/mtoto anapata haki zake zote za msingi ili kujenga familia bora….” alisema SP EG. MATIKU.
SP EG.MATIKU aliongeza kuwa Jeshi la Polisi Wilayani hapo litaendelea kusimamia Sheria kama zilivyo katika vitabu vya Sheria na Kanuni za Nchi.
“…tunatoa wito kwa wananchi wote kwa eneo langu la Ukerewe iwapo mtu yeyote kwa maksudi yake binafsi au kwa kutokujua sheria, atakayekiuka taratibu hizo, mkondo wa sheria utachukua nafasi yake, na moja ya makosa ambayo tutayashughulikia ni pamoja na mwananchi kutelekeza familia, Ushoga, Uzurulaji nyakati za Usiku, Usagaji, Wizi, Vipigo, Ukeketaji, Uvuvi Haramu, Vitendo vyote vya ukatili kwa akina Mama na Watoto na makosa mengine yanayoendana na hayo hayana nafasi katika wilaya yetu ya ukerewe….” Alisema SP EG.MATIKU.
Amewasihi wananchi waishio Nansio pamoja na waliopo katika visiwa 38 vilivyopo ndani ya eneo la Wilaya ya Ukerewe kuwa wawe katika msitari wa mbele kutoa taarifa dhidi ya vitendo viovu vinavyojitokeza kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wote.
“….wananchi wanaweza kupiga simu kwa viongozi wa Polisi kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza kwa Namba: 0739009949, Mkuu wa Polisi Wilaya Namba:0659884829, Mkuu wa Upelelezi Wilaya Namba 0744049066 au Kwa Mkuu wa Kituo Nansio Kwa Namba 0787381318….” Alisema SP EG.MATIKU.