Home Kitaifa SOKOMBI AWAOMBA WADAU KUTHAMINI MCHANGO WA WAANDISHI WA HABARI

SOKOMBI AWAOMBA WADAU KUTHAMINI MCHANGO WA WAANDISHI WA HABARI

Na Shomari Binda-TARIME

WADAU na wananchi wametakiwa kuthamini mchango wa Waandishi wa Habari kwa kazi wanazofanya za ufikishaji wa taarifa.

Kauli hiyo imetolewa na mlezi wa Waandishi wa Habari Wanawake mkoa wa Mara na aliyekuwa mbunge wa viti maalum Joyce Sokombi.

Akiwa kwenye uzinduzi wa chombo cha habari cha mtandaoni cha Dima Online Blog Nyamongo wilayani Tarime amesema Waandishi wanafanya kazi kubwa ya kufikisha taarifa lakini bado mchango wao haujathamikiwa vizuri.

Amesema kupitia Online Blog na Tv za mtandaoni wamekuwa wakifikisha taarifa kwa haraka na wananchi kuzipata kwa haraka.

Sokombi ameongeza kuwa kutokana na kazi nzuri wanayoifanya serikali inapaswa kuendelea kuthamini mchango wao na kuwaondolea vikwazo.

“Nimpongeze sana Dina Maningo kwa uzinduzi huu wa Dina Online Blog ambayo tayari imeshapewa leseni kwaajili ya urushaji wa matangazo na taarifa mbalimbali”

“Mchango wa Waandishi wa Habari ni mkubwa na ni vyema ukathaminiwa kuanzia kwa wadau,serikali na hata wananchi wanaopokea taarifa”, amesema Sokombi.

Aidha Sokombi amechangia kiasi cha shilingi milioni 1 na kuahidi kutoa camera kwaajili ya uchukuaji wa taarifa za mtandao huo.

Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo mjasiliamali Bhoke Bwiso amempongeza Dinna Maningo kwa kuanzisha mtandao huo wa habari za mtandaoni.

Amesema Mwandishi huyo amefanya kazi ya habari kwa muda mrefu na kuibua mambo ambayo yanaisaidia jamii yakiwemo ya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake mmiliki wa Blog hiyo ya Dima Online Blog,Dinna Maningo amewashukuru wale wote waliohudhuria uzinduzi huo na kuahidi kuendelea kuitumikia jamii kupitia ufikishaji wa taarifa.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mara na nje ya mkoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!