Home Biashara SOKO LA PUGU MNADANI MZUNGUKO WA FEDHA KUPUNGUA KUTOKA BILION 1.2 HADI...

SOKO LA PUGU MNADANI MZUNGUKO WA FEDHA KUPUNGUA KUTOKA BILION 1.2 HADI MILIONI 900 NA 800 KWA SIKU

Na Magrethy Katengu–Mzawa Media
Dar es salaam

BAADHI ya Wafanyabiashara wa Ng’ombe wasio waaminifu wamekua chanzo cha Upotevu wa mapato Soko la Pugu Mnadani Dar es salaam kwa kutofikisha Mifugo yao Mnadani inapotoka Mikoani badala yake kuipeleka moja kwa moja machinjioni hali iliyopelekea Soko hilo mzunguko wake kushuka kutoka billion 1.2 hadi million 900 au 800 kwa siku

Hayo yamesemwa Februari 28 ,2025 na Diwani wa Kata ya Pugu Shabani Mussa katika harambee ya kuchangisha kiasi cha fedha Tsh million 95 kwa ajili ya kujenga Jengo la Ofisi ya Chama cha Wafanyabiashara wa Ng’ombe katika soko hilo ambapo amebainisha kuwa wafanyabiashara hao kupeleka ngo’mbe zao moja moja kwa moja kwenye machinjio bila kuzitisha kwenye Mnada huo inayochangia kupungua kwa mapato na mzunguko fedha katika Mnada huo.

” Kwa kweli changamoto hii ya kupelekea ng’ombe moja kwa moja machinjioni bila kupitiasha Soko la Mnadani siyo sahihi kisheria kabisa kwani tunakosa mapato pia mzunguko wa Biashara unashuka hivyo na serikali inapoteza mapato Yake kwani kule machinjioni ushuru unatozwa kwa ng’ombe aliyechinjwa na Mnadani tunatoza ng’ombe aliye hai” amesema Diwani

Diwani Shabani mesema kisheria mifugo yote inatakiwa ifike Mnadani na yote ishushwe ili wanunuzi wanunue kisha kwenda machinjioni kufanya hivyo kutasaidia kuinua Maisha ya wafanyabiashara wa Soko hilo na mzunguko wa fedha kuongezeka.

Ameongeza amesema watakaa na wafanyabiashara kuwaeleza umuhimu wa kulipa kodi kwani changamoto zilizopo Mnadani hapo haziwezi kutatulika kama wao hawalipi kodi na maendeleo hayawezi kuonekana hivyo mikakati itawekwa na mkuu wa minada pamoja na kuzungumza na viongozi wenzake kuhakikisha ngo’mbe zote zinazofika machinjio lazima ziwe na vibali ambayo vimesaini kutoka Mnada mkuu wa Pugu na kama hazina vibali zisichinjwe.

“Hapa tumesikiliza changamoto zao wanataka maji, barabara, taa kwani mnada unafanya kazi masa 24 bila fedha za maboresho lakini haya yote hayawezi kufanyika bila wao kulipa kodi, mapato yakikusanywa lazima maendeleo yaonekane’ amesema Diwani

Naye, Meneja Mkuu wa Mnada Mkuu wa Pugu Mnadani Noel Byamungu amesema Wafanyabiashara wa Soko hilo walio wengi Hali za Maisha ya haiendani na fedha wanazozipata wanpenda starehe sanaa hiyo yote hutokana na kukosa elimu ya kifedha hivyo ameziomba Taasisi za kifedha kwenda kutoa elimu Mnadani namna ya usimamizi wa fedha kwani fedha inayopatikana kwa siku Mnadani hapo ni kati mill 800 hadi Bill 1 lakini maisha ya wafanyabiashara hao hayaendani na mzunguko wa fedha hiyo.

” Hapa Mnadani tuna tawi la benki moja tu la NMB na hufanya kazi kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa tisa Mchana huku Soko lilifanya masaa 24 wakati mwingine wanapeana fedha nyingi na usiku huo hakuna pa kuziweka wakati mwingine kuibiana” amesema Meneja

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Pugu Mnadani Edward Ntemi amesema kuwa, kulichomsukuma kuanzisha harambee za ujenzi wa ofisi ya wafanyabiashara wa Pugu Mnadani na kushirikisha wadau ni changamoto za wafanyabiashara, ikiwemo kukosa sehemu maalum ya kukutana na kutatua changamoto zao kwa faraghaa, kwani kwa sasa wanakutana popote.

“Nilipochaguliwa mwaka 2024 niliahidi wapiga kura wangu nitafanya sherehe kuwa nitachinja ngo’mbe ili tule nyama lakini nikafikiria Sana tunakulaje mama wakati hatuna Ofisi ya Chama nikakumbuka MIAKA ya nyuma kwa hayat Rais Dkt John Pombe Magufuli alivvokuwa akifanya pesa za sherehe za uhuru akazihamishia kwenye ununuzi wa vitanda vya hospital, sisi hapa hatuna ofisi nikaona ni bora pesa hizi nizihamishie kwenye kwenye ujenzi wa ofisi” amesema Ntemi

Mwenyekiti amesema kuwa wakiwa na Ofisi itawasidi kila kamati kusaidia kutatua changamoto zao Mfano mwezi unaokuja wa mfungo wa Ramadhani wageni wanaweza kufika na tukapewa tenda ya kusambaza ngo’mbe lakini wakifika hata sehemu ya kukaa kuongea Biashara hakuna inabidi tukae chini .

Aidha katika harambee hiyo walifanikiwa kuchangisha zaidi ya million tano na tayari mchoro wa Jengo tayari upo amewaomba wadau mbalimbali waendelee kuwaunga mkono kwa kushirikiana na wanachama pamoja na viongozi wenzake kufanikisha lengo lililokusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!