Na Magreth Mbinga
Hali ya mawasiliano katika mlima Kilimanjaro ipo sawa kabisa tunaishukuru sana Wizara ya Mawasiliano kupitia TTCL kwa kutoa huduma hivyo watalii wanawasiliana vizuri wakiwa juu.
Hayo yamezungumzwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Utalii Prof Eliamani Sedoyeka katika Kongamano la nne la Ushiriki wa Wanawake katika Sekta ya Utalii lililofanyika Jijini Dar es Salaam ambalo limedhaminiwa na KCB Bank.
Pia Mwenyekiyi wa Economic Society Tanzania Dkt. Tausi Kija amesema katika kongamano hilo la nne limeangazia zaidi katika ushiriki wa Wanawake katika sekta ya utalii sababu sekta ya utalii ni muhimu sana katika pato la Taifa .
“Takribani Watanzania milioni 1.6 wameajiliwa katika sekta ya utalii kwahiyo na pato letu la Taifa takribani asilimia 17 linachangiwa na sekta hii ambapo wanawake wanamchango mkubwa sana” amesema Dkt. Tausi
Aidha Mratibu wa Sneakers and Heels Zuhura Sinare Muro amesema wananafasi kubwa ya kutanua hiyo sekta ya utalii kwa wanawake na kufanya vizuri zaidi wanawake wengi wakiingia na wanaamini kabisa mwanamke akiamua akasema kwamba atatenda huwa wanakuwa na uthubutu.
“Tunamshukuru sana Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ameweka nguvu kubwa sana katika kufungua hiyo sekta na ameendesha gari la kitalii (tour car) katika filamu ya Royal Tour hiyo inawapa chachu sana wasichana na mabinti kuingia kwenye hiyo sekta”amesema Zuhura
Sanjari na hayo Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati wa Taasisi ya Trade Mark East Africa John Ulanga amesema amekuwa ni muhudhiriaji wa kila mwaka na ameona ikianza toka wazo Dk Blandina Kilama na wenzake mpaka sasa imekuwa kama taasisi inayojitegemea na kuleta watu wengi.
“Faida moja ambayo ninaiona na sababu ya Mimi kuhudhuria ni kwamba hii sio nafasi tu ya wanawake kuongea na kupeana moyo pamoja na kushikana mkono ili kuweza kukua katika kazi na nafasi zao mbalimbali lakini hii ni nafasi ambayo hata sisi wanaume tunaweza kuwaambia kwamba mnalolipanga linawezekana” amesema Ulanga
Vilevile Mkuu wa Mahusiano na Mwasiliano KCB Bank Christina Manyenye amesema wanaona umuhimu mkubwa sana kuwepo katika tukio kama hilo kwasababu wao kama Bank wanaangalia sana maswala ya wanawake kupata kipato,kuinuka kiuchumi hata kielimu ili waweze kusongambele na biashara zao.
“Kwa KCB Bank tumeona ni tukio zuri sana tumekubali kuwepo pale ili tusaidiane na kupeana ushirikianao ili tuweze kuwapeleka wanawake wa Nchi yeti mbele zaidi” amesema Manyenye.