Dar es Salaam, Agosti 16, 2022.
Kampuni inayoongoza kwa maisha ya kidijitali nchini , Tigo Tanzania imeshirikiana na Kampuni ya simu za mkononi TECNO kuzindua simu mpya za mfululizo wa TECNO , ijulikanayo kama TECNO Spark 9. Simu za kisasa za TECNO Spark 9 zinakuja zikiwa na intaneti BURE ya GB 78 kwa mwaka mzima kutoka kwa Tigo, na kuhakikisha kuwa watumiaji wanapata nafasi ya kufurahia huduma za mageuzi ya kidijitali zinazopatikana kwenye mtandao wa Tigo 4G, ambao ni mkubwa zaidi nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa TECNO Spark 9 , Mtaalam wa Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo ( Kushoto ) Bwn. Blass Abdon amesema
‘Tigo iko kwenye kilele cha mabadiliko ya mtindo wa maisha ya kidijitali. Sisi ndio waendeshaji wa kwanza na wa pekee nchini kuwa na simu za hivi punde za TECNO Spark 9 katika Maduka yetu yote ya Tigo kote Tanzania.
Blass aliongeza ‘Tigo inalenga kuendelea kuongeza kasi ya kupenya kwa simu mahiri nchini huku ikihakikisha kwamba wateja wetu wote wanafurahia matumizi bora ya kidijitali kupitia mtandao wetu wa kasi zaidi wa 4G nchini. Ndiyo maana Tigo inatoa mtandao wa GB 78 BURE kwa mwaka mzima kwa wateja wote wanaonunua simu za kisasa za TECNO Spark 9 Series.’
Akifafanua kuhusu ushirikiano huo unaosisimua, Meneja Mauzo TECNO Tanzania, Mwamvua Kapesula alisema ‘Tunajivunia sana kushirikiana na Tigo, kampuni ya simu yenye mtandao mkubwa wa 4G ili kuleta ofa za kusisimua kwa watumiaji wa Tanzania. Hii ni hatua muhimu katika maendeleo ya tasnia ya simu ambayo inaruhusu mteja kufikia simu mahiri za TECNO Spark 9 Series”.
Simu za kisasa za TECNO SPARK 9 Series zinatarajiwa kuuzwa kwa reja reja kutoka TZS 395,000/- na zinapatikana kwa ununuzi katika maduka yote ya Tigo na maduka ya TECNO kote nchini. Simu hizi za TECNO Spark 9 series zinakuja na skrini nzima ya inchi 6.6, RAM ya 4GB (RAM EXTENDABLE UPTO 7GB RAM yenye kipengele cha Memory Fusion), hifadhi ya ndani ya GB 128, kamera ya mbele ya 32MegaPixel (MP), kamera ya nyuma ya 50MP, kipengele cha kutambua uso pamoja na Warranty ya miezi 13 , Pia mteja anaponunua simu zetu atapata zawadi ya papo hapo ya Kifaa cha Kupokea sauti cha Bluetooth.