Mary Michael Isaya Mkaazi wa Dodoma akipewa zawadi na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya kati Said Iddi baada ya kununua Simu janja Aina ya ZTE katika Viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kitaifa Jijini Dodoma , Ikumbukwe Maonesho haya yanafanyika katika kanda saba (7) nchi nzima ambazo ni Kanda ya Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye uwanja wa John Mwakangale; Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere; Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye viwanja vya Ngongo; Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika viwanja vya Nyamhongolo; Kanda ya Ziwa Mashariki mkoani Simiyu katika viwanja vya Nyakabindi; Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye viwanja vya Themi; na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye viwanja vya Fatma Mwasa , na Kampuni ya Tigo inashiriki katika Kanda hizo zote.
Na Adery Masta.
Kampuni namba moja nchini kwa utoaji wa huduma za Kidigitali Tigo Tanzania , kama ilivyo miaka yote imeendelea kushiriki , Maadhimisho na Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane) yanayofanyika Kitaifa jijini Dodoma , Katika Maonesho hayo Kampuni ya Tigo inaendelea na Kampeni yake ya SAKO KWA BAKO yenye lengo la kurudisha kwa wateja wao ambao wameuchagua mtandao wa Tigo , ambapo kupitia Kampeni hii wateja wanapata zawadi mbalimbali wanaponunua vifurushi vya Tigo.
Aidha , Katika maonesho haya Kampuni ya Tigo wamekuja na Simu ya Bei nafuu ya ZTE , akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kati Said Iddi amesema
” Kampuni ya Tigo imewaletea wananchi na wadau wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi simu hii ya ZTE ambayo inatolewa kwa Mkopo na kianzio kikiwa na Tsh. 35000 ( Elfu Thelethini na Tano ) na baada ya hapo mteja atalipa 650 tu kwa siku , Lengo la kuleta simu hii tunataka kuwawezesha wananchi , wakulima na Wavuvi kuweza kupata taarifa sahihi za shughuli zao kwa maana tukimpa simu janja kwa bei nafuu anakua na uwezo wa kutembelea mitandao mbalimbali na kutafuta anachokitaka kwa wakati hasa kupitia mtandao wetu wenye kasi zaidi “
Kwa taarifa zaidi tembelea Banda lolote la Tigo lililopo katika Maonesho ya Nane Nane katika Kanda zote tajwa hapo juu.