Magrethy Katengu
Klabu ya Mpira ya Simba imesema itaendelea kuweka kumbukumbu za taarifa pamoja na Vielelezo vya klabu hiyo kwenye Makao Makuu Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za makumbusho ya taifa Afisa Habari wa klabu hiyo Ahmed Ali amesema Vielelezo vya timu hiyo na Historia ya timu hiyo ikiwemo kibegi cha Simba kuwekwa cha kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo 1936 na siku za mbeleni historia hiyo itapatikana kwenye Makumbusho ya taifa.
“Kuanzia Sasa historia ya timu ya Simba na Vielelezo vyake ikiwemo kibegi cha Simba kitapatikana katika makumbusho ya taifa na tutaendelea kuleta nyaraka nyingine “.amesema Msemaji wa Simba Ahmed Ally.
Ahmed Ally amesisitiza historia ya Mwaka 1936 ya Tangu kuanzishwa kwa timu ya Simba utapatikana Kwenye Makumbusho ya taifa.
Aliongeza katika kuelekea Maadhimisho ya Simba Day Jumapili wanamtarajia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Mgeni Rasmi wa tukio la Simba Day.