NA Magrethy Katengu
SILENT OCEAN kampuni ya Usafirishaji imekuja na suluhisho la usafirishaji mizigo kutoka nchini India kwa muda kuanzia siku 17-25 ambapo hapo awali mizigo ilikuwa ikisafirishwa hadi kufika Tanzania ilikuwa ikitumia miezi 3 hali iliyokuwa ikisababisha bidhaa nyingine kufika zikiwa zimepoteza ubora na kupelekea hasara.
Ameyasema hayo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Mohammed Soloka wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofisi Mpya iliyoanzishwa Mumbai nchini India, amebainisha kuwa wamesogeza huduma bora kwa wafanyabiashara wanaotoa bidhaa zao nchini India na kusafirisha kwa njia ya bahari na kuelekea nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania, Marekani, China kwa muda mfupi .
“Kampuni yetu ya Silent ocean iliona kwa jicho la mbali jinsi wafanyabishara adha waliyokuwa wanapitia kwa kusafirisha mizigo kwa muda mrefu na bidhaa zao nyingine zilifika zikiwe zimepoteza ubora hivyo kwakua India ni nchi ya pili duniani inayokua kwa kasi katika biashara na tuliona changamoto ya kuchelewesha kwa mizigo kufika nchini tukaamua kufungua ofisi hii,” amesema Soloka.
Amesema siku zote wapo na wafanyabiashara na kwamba hiyo ni fursa kwa Serikali kukusanya mapato na kukuza uchumi wa nchi kupitia ofisi hiyo na wafanyabishara watasafirisha mzigo kutoka India hadi Tanzania
Mfanyabiashara wa bidhaa za Viatu Mitandio, nguo za kihindi Wahidi Abdul amesema hapo awali kabla ya Silent ocean walikuwa wanapa adha ya kusafirisha mizimo yao kwa gharama ya juu kwa njia ya ndege wakitaka ifike na ndege inachagua mizigo ya kusafirisha hivyo ufumbuzi umepatikana
“Usafirishaji mizigo kwa njia ya ndege ni lazima ununue begi utalalofuatana nalo linagharimu dola za marekani milioni 80-50 hivyo inampa uzito mtu mmoja kubeba mabegi manne au matano hivyo kampuni hii imekuja na ufumbizi wa changamoto hii tuliyokuwa tunateseka kwa muda mrefu“
Naye SADA Malkanza Mfanyabiashara wa Urembo, vitu vya Watoto na mitandio amesema SILENT ocean ni Simba wa bahari ambao ni muarobaini wa kusaidia Wafanyabishara kusafirisha bidhaa kwa muda mfupi kutoka Tanzania hadi India bila usumbufu.
Nae Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabishara Kariakoo, Abdalah Mwinyi amesema wana haki ya kuwashukuru Silent Ocean kutokana na kurahisisha na kufika kwa wakati mizigo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
“Siku hizi mbili tunapitia kwenye wakati mgumu tunaimani kikao cha kesho na Waziri Mkuu kitaleta matunda, tunashukuru Silent Ocean kwa kuongeza tawi lingine,”.
Naye Mwakilishi wa Wafanyabishara, Wahid Abdulghafoor amesema wafanyabishara wa nchi hizi mbili walikuwa na changamoto ya usafirishaji wa mizigo hivyo kwa sasa wanahitaji kufanya kazi na Silent Ocean.