Home Kitaifa SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKATILI KWA WAZEE KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MARA

SIKU YA KIMATAIFA YA KUPINGA UKATILI KWA WAZEE KUFANYIKA KITAIFA MKOANI MARA

Na Shomari Binda-Bunda

Katika kuadhimisha siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee kimataifa juni 15, 2024, kitaifa yatafanyika katika mkoa wa Mara ambapo kabla ya kikele hicho kutafanyika zoezi la upimaji wa afya kwa wazee pasipo gharama yoyote juni 13 kwenye uwanja wa shule ya msingi Miembeni.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Gerald Kusaya katika mkutano wake na waandishi wa habari ukiofanyika juni 04 mjini Bunda.

Aidha Kusaya amesema zoezi hilo la upimaji litaongozwa na mganga mkuu wa mkoa wa Mara na wataalam wa afya wa hospital ya rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na wengine kutoka Bunda, baada ya zoezi hilo jioni yake kutafanyika matukio ya michezo mbalimbali itakayo wahusisha wazee.

Katika kuelekea siku hii ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo kitaifa itafanyika mkoani kwetu hapa wilayani Bunda itatanguliwa na matukio mbalimbali, suala la afya ni jambo la msingi na wazee wetu watapimwa na kuchunguzwa afya zao bure juni 13 kwenye uwanja wa shule ya msingi Miembeni” amesema

Vilevile Kusaya amesema siku ya juni 14 kutafanyika kongamano mjini Bunda kuzungumzia athari za matukio ya ukatili dhidi ya wazee na namna ya kupambana nayo ambapo mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi ataongoza kongamano hilo.

Aidha Kusaya amesema Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Doroth Gwajima atakuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho hayo.

Kusaya amewahimiza wakazi wa Mara kujitokeza kwa wingi kushiriki katika matukio haya muhimu na kuonyesha mshikamano wao kwa wazee. “Ni jukumu letu sote kuhakikisha wazee wanapata heshima wanayostahili,” alisisitiza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!