Home Kitaifa SIKIKA WATOA MATOKEO YA UTAFITI WA UWAZI NA UWAJIBIKAJI WA WANANCHI KATIKA...

SIKIKA WATOA MATOKEO YA UTAFITI WA UWAZI NA UWAJIBIKAJI WA WANANCHI KATIKA MASWALA YA BAJETI

Na Magreth Mbinga

Taasisi ya SIKIKA imetoa matokeo ya utafiti ambao umefanyika mwaka 2020 juu ya uwazi na uwajibikaji wa mwananchi katika maswala ya bajeti.

Matokeo hayo yamewasilishwa na Program officer SIKIKA Godfrey Mfumu na kusema kuwa utafiti huo wamefanya katika halmashauri saba na katika kila halmashauri waliweza kutembelea kituo kimoja Cha kutolea huduma za afya au zahanati.

“Katika utafutaji wa taarifa tulianzia halmashauri tuliangalia mbao za matangazo kuna taarifa gani na baada ya hapo tulienda katika vituo vya kutolea huduma za afya na shule kwa kila halmashauri ambayo tulikuwa tumeenda”amesema Mfumu.

Pia Mfumu amesema kulikuwa na changamoto za upatikanaji wa nyaraka muhimu ambapo mwananchi akienda kwenye ofisi za halmashauri na kuomba kupewa taarifa watendaji wanakuwa na wasiwasi anataka akazifanyie nini kitu ambacho kina kinzana na sheria ya haki ya upatikanaji wa taarifa .

Aidha Mchumi Idara ya Serikali za Mitaa Tamisemi Stella Sasita amesema kwao Tamisemi ni fursa njema kuona ni namna gani wananchi wanashiriki na wanawajibika vipi katika maswala mazima ya bajeti.

Sisi Tamisemi tunatekeleza programu ya fursa na vikwazo kwa maendeleo ni fursa nyingine ya kujua na kujifunza kwamba kule chini jamii imehamasika kwa namna gani kuhusu maswala mazima ya upangaji wa bajeti”amesema Sasita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!