Home Kitaifa SHULE YA KWANZA YA GOROFA YA SEKONDARI KUJENGWA KATA YA KIGERA MANISPAA...

SHULE YA KWANZA YA GOROFA YA SEKONDARI KUJENGWA KATA YA KIGERA MANISPAA YA MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

SHULE ya kwanza ya sekondari ya gorofa itaanza kujengwa hivi karibuni Kata ya Kigera manispaa ya Musoma.

Ujenzi huo utaanza baada ya hii leo januari 15 Meya wa manispaa ya Musoma Kapteni mstafu Patrick Gumbo kumuonyesha mkandarasi eneo la ujenzi ilipo Mwiyale sekondari.

Akizungumza kwenye eneo hilo Gumbo amemtaka mkandarasi kuanza ujenzi mara moja ili kuendelea kutoa fursa ya watoto kupata elimu.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ni matokeo mazuri ya kazi inayofanywa na Rais Dkt.Samia katika kuinua sekta ya elimu.

Gumbo amesema shule za gorofa zimekuwa zikionekana katika maeneo mengine na sasa ni zamu ya kuing’alisha manispaa ya Musoma.

” Eneo la ujenzi hili hapa ni imaani yangu ujenzi utafanyika kwa wakati kutokana na mkataba wa ujenzi unavyoelekeza.

” Tunashukuru serikali ya Rais Dkt.Samia kwa kuendelea kutuletea fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu”,amesema.

Diwani wa Kata ya Kigera Alex Nyabiti ameishukuru serikali na halmashauri ya manispaa ya Musoma kupeleka mradi huo kwenye Kata yake.

Amesema kujengwa na kukamilika kwa shule hiyo kutawezesha watoto wengi kupata mahala sahihi na bora pa kupata elimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!