Home Kitaifa SHIVYAWATA WALIA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOWAKABILI.

SHIVYAWATA WALIA NA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZOWAKABILI.

Theophilida Felician Kagera.

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera waelezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo watu wenye ulemavu katika maisha.

Wameyaeleza hayo baadhi wakishiriki mjadara wakuyabainisha masuala kadha wa kadha yanayohusu kundi hilo ambapo majadiriano hayo yamefanyika katika viunga vya ofisi yao iliyopo Manispaa ya Bukoba.

Mada kuu ilikuwa nikutizama hali ya ushiriki na ushirikishwaji katika masuala mazima ya kijamii kwa watu wenye ulemavu kwa lengo la kuona ni jinsi gani watu wanamna hiyo wanashiriki nakushirikishwa kikamilifu kupitia nyanja tofauti tofauti za kijamii.

mada hiyo baada ya kuwasilishwa na mtoa mada Mugisha Kasaaju mtalaamu wa masuala ya jamii imeyaibua mengi yenye changamoto nyingi zinazowasibu kimaisha ambapo wengi wao wamefikia hatua ya kutamka wazi juu ya kukata tamaa kutokana na adha wanazokumbana nazo.

Dativa Pastory mkazi wa mtaa wa Nyakanyasi kata Bakoba ni mzazi wa mtoto mlemavu Egibathi Egidius mwenye umri wa miaka 15 tangu kuzaliwa kwake hawezi kukaa wala kusimama ametelekezwa na mzazi mwenzake mtoto huyo akiwa na mwaka mmoja hivyo amehangaika mno katika kuhakisha ana shiriki malezi ya mtoto wake huyo Egibathi.

Amefafanua kuwa anakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya uhaba wa mahitaji ya kujikimu japo amekuwa akipambana huku na kule ili kufanikiwa chochote cha kumtunza yeye na mwanaye.

“Mwanangu huyu hakai, hasimami, hatembei wala haongei na mimi ndo mama ndo baba nafika hatua nashindwa la kufanya wakati mwingine huumwa matibabu shida changamoto ni rukuki naumia sana kuona hali hii ya maisha yangu na mwanangu” ameeleza mama huyo huku akibubujikwa na machozi mbele ya washiriki

“Wanasema walemavu wana misaada sijawahi kuona msaada huo nimefika hata ofisi za Manispaa lakini sijafanikiwa kitu mpaka leo hii niliomba kuingizwa hata TASAF ikashindikana , mimi njia ambayo inaweza kunisaidia ningepata shughuli ya kukaa sehemu moja nikatulia nikafanya biashara hata ndogo ndogo baada ya kupata mtaji inaweza kunisaidia hiyo kazi za kutembea zinaniwea ngumu kutokana na kutumia muda mwingi wakumlea mwanangu” ameendelea kusema Dativa Pastory.

Naye mzee Sarapioni Rugayana mlemavu wakutokuona amesema kwamba wao kama watu wenye ulemavu bado wanazipitia changamoto japo Serikali hususani ngazi ya juu inapambana kuzitatua ila kwa ngazi za chini kuanzia vijiji , mitaa bado hawaonwi kabisa make hata mfano viongozi wamaeneo husika wakiulizwa idadi ya watu wenye ulemavu siyo jambo jepesi kuwa na idadi yao kamili jambo ambalo linaweka wazi kuwa hawatilii maanani juu ya kulishughulikia kiukaribu kundi hilo.

Ameeleza kwamba imefikia hatua ya wao kukata tamaa kabisa kwa kila jambo.

Katika kikao hicho wametoa mapendekezo kwa Serikali wakiiomba kuyatekeleza masuala mbalimbali ya watu wenye ulemavu ikiwemo ya kuundwa jumuiya ya watu wenye ulemavu kwa Imani kwamba itasaidia kuzitatua changamoto zao kwa undani badala ya kujumuishwa katika makundi mengine, pia nakuona umuhimu wakuwahusisha kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF kwani umekuwa ukiwapita pembeni watu wenye ulemavu walio nahali ngumu kimaisha.

Kikao hicho kimehudhuriwa na vyama ambavyo ni CHAWATA, TLB, TAS, CHAVITA na TAMU chini ya Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Bukoba Novati Joseph Mwijage kimeyagusia mambo mengi yakiwemo ya kisiasa, kiafya, kielimu, kiuchumi na mengineyo.

Mbali na hayo hawakusita kutoa pongezi kwa serikali wakisema kuwa licha ya changamoto bado Imeyatekeleza mambo kadhaa yakuzitatua changamoto hizo kwa kiasi chake ambapo wameiomba kuendeleza jitihada hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!