Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji Nchini Tanzania leo Septemba 22, 2024 wametoa msimamo wa kutokushiriki maandamano ambayo yamepangwa kufanyika siku ya Septemba 23, 2024 Mkoani Dar Es Salaam yaliyotangazwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Msimamo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji kwaniaba ya wanachama wote Nchini na kusema kuwa tunu ya amani ya Nchi ni kubwa kuliko kitu chochote hivyo hawawezi kuishi kwa wasiwasi endapo wataandamana hawataweza kuthamini mali zao.
Pia Katibu wa Shirikisho hilo Michael Liganya amesema wakishiriki maandamano hayo watakuwa wametengeneza matatizo makubwa kwa sasa katika Nchi ya Tanzania bodaboda hawapo tayari kuwa miongoni mwa wavunjifu wa amani.
Aidha msemaji wa Shirikisho la waendesha bodaboda na bajaji Tito Lazaro amesema hakuna bodaboda atakae andamana siku ya Septemba 23 hivyo wataendelea na shughuli zao za kila siku zinazowawezesha kupata kipato na kuendesha maisha yao.