Home Kitaifa SHIRIKA LAKABIDHI BOTI KWA AJILI YA ULINZI RASILIMALI BAHARI.

SHIRIKA LAKABIDHI BOTI KWA AJILI YA ULINZI RASILIMALI BAHARI.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Said Khalid (mwenye kipaza sauti) akikabidhi Boti ya Ulinzi Shirikishi kwa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari kata ya Boma wilayani Mkinga mkoani Tanga Leo

Na Boniface Gideon, Mkinga

Wakazi wa Vijiji 5 kati ya 9 vilivyopo kata ya Boma wilayani Mkinga mkoani Tanga vimenufaika na Mradi wa utunzaji wa Rasilimali Bahari unasimamiwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Baada ya leo kukabidhiwa Boti kwaajili ya kuongeza Ulinzi Shirikishi kwa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari za CFMA na BMU.

Boti hiyo inathamani ya Mil.35 imetolewa kwa Vijiji vya Boma kichakamiba,Mwaboza,Boma Subutuni na inaelezwa itasaidia kwakiasi kikubwa kulinda Rasilimali Bahari ikiwemo kuzuia uvuvi haramu .

Boti hiyo imekabidhiwa ikiwa ni miezi michache imepita Baada ya Wavuvi na wakazi wa Vijiji hivyo kupatiwa Elimu ya Ufugaji wa miamba Bahari ambayo imesaidia Wavuvi kuvuna Samaki Wengi aina ya pweza kila Baada ya siku 90 kwa kupitia njia ya ufungaji wa miamba Bahari.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Shirika Hilo Said Khalid alisema Boti hiyo itawasaidia wakazi wa Vijiji kuongeza Ulinzi Shirikishi Baharini,

Boti hii itasaidia kuongeza Ulinzi Shirikishi wa Rasilimali Bahari,lengo kubwa nikuhakikisha Rasilimali Bahari zinawainua Kiuchumi wakazi wa Vijiji hivi” Alisema Khalid

Khalid alisema wataendelea kutoa Elimu ya Mazingira kwa wakazi wa Vijiji kata hiyo,

Shirika letu litaendelea kutoa msaada wa Vifaa kazi na Elimu ya Mazingira na tutaendelea kushirikiana na Serikali,wakazi wa Vijiji hivi katika kuhakikisha Bahari inawaletea manufaa wakazi wote hususani Wavuvi” Alisisitiza Khalid

Akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu alilishukuru Shirika Hilo kwa msaada huo nakuwataka Wadau mbalimbali kuendelea kuisaidia Jamii ya Mwambao wa Bahari ili Matumizi ya Bahari yaweze kuleta matokeo chanya ya Kiuchumi kwa wakazi,

“‘kwaniaba ya Wakazi wa Wilaya ya Mkinga tunatoa Shukrani Sana kwa msaada huu tunawaahidi kuwa msaada huu utatumika kama ilivyokusudiwa , niwaombe Wakazi wa Boma hususani Wavuvi nendeni mkaitumie Boti hii kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo ” Alisema

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Jumuiya za Usimamizi wa Rasilimali Bahari CFMA ( BMU) Wilaya ya Mkinga Kassimu Alfan alishukiru msaada huo nakwamba awali kabla ya kupokea msaada huo walikuwa wanatumia mitimbwi na majahazi kufanya doria za Ulinzi Baharini Hali iliyowawia vigumu kuwapata wahalifu,

Awali tulikuwa tunateseka Sana kufanya Ulinzi Baharini kutokana na kukosa Vifaa vya kisasa kwakuwa wahalifu Wengi wa Baharini wanatumia Boti za kisasa hivyo ilikuwa ni vigumu kuwakamata kirahisi lakini kwasasa tutawakamata kwa urahisi kwakuwa tunavifaa vya kisasa zaidi

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!