Home Burudani SHINDANO LA MISS HIGHER LEARNING LA ZINDULIWA RASMI 

SHINDANO LA MISS HIGHER LEARNING LA ZINDULIWA RASMI 

MASHINDANO ya Ulimbwende kwa ngazi ya vyuo “Miss Higher Learning ” yawaomba wanafunzi vyuoni kujijengea uthubutu wa kushiriki shindano hilo lenye kufungua milango  mingi ya fursa mbalimbali kwa warembo waliopo vyuoni.

Akizungumza wakati wa Kuzindua rasmi Msimu mwengine  wa shindano hilo Leo, Februari 04,2023 Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Kamati ya Shindano hilo Adam Nkundia amesema  Shindano hilo limeacha alama nyingi na kufungua fursa nyingi katika makampuni nje na ndani ya nchi kwa warembo ambao wameshiriki shindano hilo.

Warembo wamekuwa na fursa nyingi ikiwa kuwa mabalozi kwenye makampuni ikiwemo kampuni ya nywele ambayo ndio wadhamini wa shindano wakitangaza aina mbalimbali ya nywele hizo kwa mkataba wa mwaka mzima “.

Hata hivyo Nkundia amewaomba wadau na wadhamini kujitokeza kwa wingi kudhamini shindano hilo ambapo usahili utafanyika rasmi Februari 11,2023 ukumbi wa a hug Mug Masaki huku Fainali ikitarajiwa kuwa rasmi mwezi Machi.

Kwa upande wake Miss Higher 2022 Otaigo Mwema ambae anamaliza muda wake amesema kupitia jukwaa hilo la “Miss Higher Learning ” limemjengea uthubutu wa kukutana na wadau mbalimbali ambao hakutegemea kukutana nao.

“Mwanzo wakati nashiriki shindano hili nilikuwa muoga zaidi lakini baada ya kujifunza vingi pamoja na kujiamini mbele ya jamii kuwa nipo kwa ajili ya kulibeba taji hili kama Mrembo msomi.”

Pia Mwema amewaomba wadau kujitokeza kudhamini shindano hilo kwa lengo la kunyanyua vipaji vya mabinti hao mashuleni. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!