Home Michezo SHINDANO LA KUENDESHA PIKIPIKI KUKUSANYA WASHIRIKI NDANI NA NJE YA NCHI

SHINDANO LA KUENDESHA PIKIPIKI KUKUSANYA WASHIRIKI NDANI NA NJE YA NCHI

Shindano la kuendesha pikipiki ambalo linajulikana kwa jina la EAST AFRICA SAN VILLAGE litafanyika tarehe 17 Kibaha Misugusugu katika uwanja wa shule ya msingi.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa DRMSC Ahmed Abdalla ambao ni waandaaji wa mashindano hayo na kusema kuwa siku ya tarehe 16 watakuwa wanapokea washiriki .

Pia Ahmed amesema mashindano hayo yataanza saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo wanaotarajia kushiriki ni watu 60 ambapo 40 wanaotumia pikipiki maalum za mashindano na 20 bodaboda kutoka Mikoa mbalimbali ya Tanzania bara ,visiwani na Nchi jirani ikiwemo Kenya na Uganda.

Tumeandaa mazingira mazuri kwaajili ya mchezo huo kutakuwa na maeneo ya mchanga, tope, kona nyingi na matuta makubwa kwaajili ya kurusha pikipiki “amesema Ahmed.

Aidha Katibu wa DRMSC Bazdawi Alsuqry amesema wameandaa mchezo huo kwania ya kuwakusanya waendesha pikipiki katika uwanja mmojaekuonyesha uwezo wa kucheza na pikipiki wasifanyie mitaani ambapo wanaweza sababisha madhara kwa jamii inayowazunguka.

Sanjari na hayo mtu wa usalama wa mchezo huo Yusuph Maguo amesema kwa upande wa usalama wamejipanga vizuri kutakuwa na gari ya wagonjwa, zimamoto na watu wa huduma ya kwanza kwaajili ya kuhudumia wachezaji na watazamaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!