Home Kitaifa SHILINGI BILIONI 4.2 KUJENGA DARAJA JIPYA LA MSADYA, MPIMBWE MKOANI KATAVI

SHILINGI BILIONI 4.2 KUJENGA DARAJA JIPYA LA MSADYA, MPIMBWE MKOANI KATAVI

Serikali kupitia Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kujenga daraja jipya la Msadya lililopo kata ya Mwamapuli, Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe mkoani Katavi.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff katika ziara yake mkoani Katavi ambapo mwez Mei 2022 ambapo alitembelea Halmashauri za Mpimbwe na Mlele.

Ujenzi wa Daraja jipya la Msadya utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.2 na Mkandarasi Mshauri atakayesimamia atalipwa shilingi milioni 450. Kwa sasa mkandarasi analeta vifaa vyote hapa na tunategemea ataanza kazi baada ya wiki moja, “ alisema Mhandisi Seff.

Pia alieleza kuwa kazi ya ujenzi wa daraja hilo inategemewa kukamilika katika kipindi cha miezi 18 na daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 60.

Naye Diwani wa Kata ya Mwamapuli Mhe. Edward Nyorobi alisema kuwa daraja hilo linalounganisha Kata za Mwamapuli na Chamalendi ni muhimu sana kwa wananchi kwa ajili ya kusafirisha mazao yao na kukuza shughuli za kibiashara na uchumi.

Kata hizi zinategemewa sana kwa kuzalisha chakula na kukuza mapato ya hapa na Halmashauri nzima. Kuna hekari zaidi ya 13000 za uzalishaji wa mazao, tunamshukuru sana Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea pesa za daraja hili ambalo litakuwa mhimili na mkombozi kwetu,“ alisema Mhe. Edward.

Kwa upande wake ndugu Hansi Mlange mkazi wa Mwamapoli alisema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja la muda baada ya daraja la awali kuvunjika na kueleza kuwa daraja jipya litakalojengwa litakuwa ni suluhisho la kero zao za muda mrefu.

Tunachoiomba Serikali ni kutujengea Daraja la viwango litakaloweza kubeba kuanzia tani 30 ili liwe na faida kubwa kwetu katika kusafirisha mazao,” alisema Hansi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!