Home Kitaifa SHEKH MKOA WA SIMIYU ACHANGIA UJENZI WA MADRASA MUSOMA AKIONGEA KWA SIMU...

SHEKH MKOA WA SIMIYU ACHANGIA UJENZI WA MADRASA MUSOMA AKIONGEA KWA SIMU NA MEYA GUMBO

Na Shomari Binda-Musoma

SHEKIKH wa mkoa wa Simiyu Issa Kwezi Kidayi amechangia mifuko 10 ya saruji kwenye ujenzi wa madrasa kwenye Msikiti wa Mwisenge na kusisitiza elimu ya dini kwa watoto.

Akitoa ujumbe wa Sheikh huyo kwenye kisomo cha Maulid kulichofanyika msikitini hapo Shekh Yakub Saburi aliyemwakilisha amesema suala la elimu kwa watoto ni mambo yaliyoimizwa na Shikh Issa.

Amesema kupitia madrasa watoto wanafundishwa elimu ya dini na kuwa na malezi bora yanayompendeza Mwenyezi Mungu.

Sheikh Issa amesema ni vyema jamii kujikita katika kuchangia mambo ya heri kuliko kujikita zaidi kwenye dunia.

Amesema watoto wanaposomeshwa elimu ya dunia ni muhimu pia kuijua akhera yao ambayo wataipata kupitia madrasa.

” Sheikh alitamani sana kufika kwenye hadhara hii na ilikuwa tuje nae lakini amepata udhuru hivyo hakuweza kufika na tumekuja kumuwakilisha”,amesema Sheikh Yakub.

Akizungumza kwa njia ya simu na Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo aliyekuwa mgeni rasmi na kuendesha harambee hiyo Sheikh Issa amesema anachangia mifuko 10 ya saruji na kuongeza kuwa upendo ni muhimu kwenye jamii.

Kwa upande wake Meya Gumbo aliyongoza harambee ya ukamilishwaji wa madrasa hiyo amemshukuru Sheikh huyo wa mkoa wa Simiyu kwa upendo wake wa kuhakikisha watoto wa Mwisenge wanapata madrasa ya kujifunza dini.

Sheikh wa mtaa wa Mwisenge Amani Kapama amewashukuru wote waliochangia sehemu ya ujenzi wa madrasa hiyo na kumuomba Mwenyezi Mungu kuwazidishia walipotoa.

Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi milioni 3,265,000 kilipatikana huku Meya Gumbo na mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo wakuchangia shilingi milioni 1,171,000

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!