Na Shomari Binda_Musoma
SHEIKH wa Wilaya ya Musoma Abubakar Mukama amemshukuru Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa Mgore Miraji kwa kuwa mstari wa mbele kuchangia masuala ya dini.
Shukrani hizo amezitoa leo januari 25 kwenye Msikiti wa Kigera bondeni ilipokuwa ikisomwa Maulid iliyoambatana na harambee ya uchangiaji kukamilishwa kwa upanuzi wa Msikiti huo.
Amesema mara kadhaa amekuwa akimsikia kiongozi huyo akichangia masuala ya dini hivyo hakuna budi kumshukuru kwa anachotoa
Sheikh Abubakar amesema ni wanaojitoa kuchangia masuala ya dini na kurudisha shukrani kwao inawatia moyo na kutoa hamasa kwa wengine kuchangia
Amesema mifuko 20 ya saruji iliyotolewa na kiongozi huyo sio midogo na itasaidia sehemu ya ujenzi katika ukamilishwaji wa msikiti huo.
” Tunamshukuru mheshimiwa Mgore Miraji ametuchangia mifuko 20 ya saruji kwenye kukamilisha upanuzi wa Msikiti uliopo mbele yetu.
” Huu sio mchango mdogo na itapendeza kila mmoja akiwa sehemu ya kuchangia ili kuweza kuukamilisha na kupata sehemu sahihi pa kufanya ibada.
Katika hatua nyingine Sheikh Abubakar amewataka waumini ya dini ya kiislam kuwa na mapenzi na kujitoa kuchangia masuala ya dini
Amesema kwa nafasi yake kama Shekh wa Wilaya atahakikisha umoja na mshikamano unakuwepo baina ya waumini na jamii maeneo ya misikiti