Home Kitaifa SHANGWE LA WASHINDI WA MAGIFTI DABO DABO WIKI YA NNE, WAMWAGIWA MAMILIONI

SHANGWE LA WASHINDI WA MAGIFTI DABO DABO WIKI YA NNE, WAMWAGIWA MAMILIONI

 Disemba 22, 2023 , Ramla Athuman Kopwe Mkazi wa Kigogo Fresh Chanika, Rosa Leonard Mchome Mkazi wa Changanyikeni Dar Es Salaam, na Raphia Abdulaziz Tendega Mkazi wa Tabata Dar Es Salaam wameingia kwenye Orodha ya Washindi 60 hadi hivi sasa wa zawadi na Mamilioni ya Fedha kutoka kampeni ya MAGIFTI DABO DABO , ambapo wao wameshinda Milioni moja kila mmoja.

Ikumbukwe Kampeni hii inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo imezinduliwa mwishoni mwa Novemba  huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) , kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.

Akizungumza baada ya kuwakabidhi mfano wa Hundi washindi hawa  Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha  amewasisitiza Watanzania kufanya miamala mbalimbali na Tigo Pesa ili kuibuka washindi maana kampeni bado inaendelea

” Muda huu tunaozungumza kuna washindi 15  wametoka DUBAI, na  wengine wamerudi wiki iliyopita kutoka Zanzibar lakini bila kusahau kuna wengine wamejishindia Pesa Taslimu na wapo pia wamejishindia Vifaa vya Hisense kwahiyo kampeni bado inaendelea fanyeni miamala na TIGO PESA kwa wingi, Lipa kwa Simu, nunua vifurushi ili utengeneze mazingira ya kuibuka Mshindi ” alisema Mary Rutha .

Wakizungumza kwa nyakati tofauti washindi wameipongeza tigo kwa kuwakumbuka wateja wake kupitia kampeni mbalimbali, Aidha wamewasihi watanzania kufanya miamala na Tigo Pesa maana ndo Siri pekeee ya Ushindi, wameongezea kuwa Fedha hiyo waloshinda itawasaidia kuongeza mtaji katika biashara zao ndogo ndogo wanazozifanya lakini pia watatenga kiasi kwa ajili ya kusheherekea sikukuu za Krismas na Mwaka mpya na wawapendao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!