Home Kitaifa SHAKA: RAIS SAMIA AMEFUNGUA MATUMAINI MAPYA, FURAHA KWA WATANZANIA

SHAKA: RAIS SAMIA AMEFUNGUA MATUMAINI MAPYA, FURAHA KWA WATANZANIA

Dar es Salaam

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa(NEC) ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Itikadi na Uenezi Ndg.Shaka Hamdu Shaka amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya kwa Taifa ikiwemo kufungua matumaini mapya, furaha na mwanga wa maendeleo kwa wananchi.

Shaka ametoa pongezi hizo leo Novemba 5,2022 wakati wa Kongamano maalum la kumpomgeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia Watanzania katika maendeleo ambalo limeandaliwa na Jukwaa Jamii Mpya.

Uongozi wake umefungua matumaini mapya kwa Watanzania, furaha na mwanga wa maendeleo kwao. Lengo kuu la Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 ni kumkomboa mwananchi kutoka katika wimbi la umasikini. Katika kipindi chake cha Mwaka mmoja na miezi minane tunampogeza Rais Samia kwa kuimarisha diplomasia yetu kwa mataifa jirani na mataifa ya nje katika sekta za kiuchumi na kisiasa”

“Rais Samia amezitembelea nchi takribani 22 kwa zaidi ya awamu 25 nchi yetu imeendelea kufunguka kiuchumi kupitia biashara na nchi za nje. Takwimu za hivi karibuni zimerekodi ongezeko kubwa la mauzo ya nje kwa bidhaa na huduma za Tanzania katika nchi mbalimbali za Afrika Mashariki,” alisema.

Ameongeza takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu ya nchini Kenya (Kenya National Bureau of Statistics) zimeonesha kukua maradufu kwa mauzo ya Tanzania katika nchi huiyo kwa takribani sh. bilioni 20.5 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2021/2022 kutoka sh. bilioni 10.8 kwa mwaka uliopita wa 2020/2021.

Nitumie fursa hii pia kumpongeza Rais Samia kwa ziara yake ya China ambayo imeitimishwa Jana tarehe 4, Novemba, 2022. Tumeshudia mikataba ya ushirikiano ikisainiwa kuna mikataba ya ushirikiano biashara, uwekezaji, uchumi wa kidigitali, ushirikiano katika maendeleo, masuala ya mazingira, uchumi wa bluu na kubadilishana uzoefu katika nyanja ya sayansi na teknolojia,” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!