Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka amewasili mkoani Tabora kwa ziara ya siku tano kuanzia tarehe 16-20 Agosti, 2022 yenye lengo la kuimarisha uhai wa chama, kufuatilia na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020-2025 pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Shaka amepokelewa katika uwanja wa ndege Tabora na kamati ya siasa ya mkoa wa Tabora pamoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Mheshimiwa Balozi Batilda Burian.
Baada ya mapokezi hayo alipata nafasi ya kuvishwa skafu na vijana wa itifaki pamoja na kukutana na kamati ya siasa ya mkoa ambapo alipokea taarifa za kazi kwa chama na serikali na baadae leo ziara yake itaanzia wilaya ya Kaliua.
Katika ziara hiyo Shaka ameambatana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya CCM ya Wazazi Tanzania Ndg Gilbert Kalima.