Home Biashara SERIKALI YAZIDI KUIHAKIKISHIA USHIRIKIANO SEKTA BINAFSI

SERIKALI YAZIDI KUIHAKIKISHIA USHIRIKIANO SEKTA BINAFSI

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amesema Serikali inathamini mchango wa sekta binafsi katika kuwekeza na itaendelea kushirikiana nayo ili wananchi waweze kupata huduma iliyobora ili kukuza uchumi wa nchi.

Kigahe ameyasema hayo Juni 23, 2022
wakati hafla ya maadhimisho ya miaka 30 ya ushirikiano kati ya Kampuni ya ‘Superdoll’ na kampuni kubwa inayoongoza duniani kwa utengenezaji wa matairi ‘Michellin’ yenye Makao Makuu yake nchini Ufaransa yaliyofanyika katika
ofisi za Kampuni hiyo,Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa ushirikiano kati ya Superdoll na Michellin ambapo kwa hivi sasa katika miaka 30 ya uwekezaji wameweza kuja na teknolojia mpya ya matumizi ya mataili ya tubulesi ambayo
yameleta mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji hapa nchini.

“Ni asilimia 98 ya Tanzania inatumia tubules tofuti na nchi nzingine, nawapongeza mlipofikia hii ni hatua kubwa, “Serikali ipo na itaendelea kushirikiana na sekta binafsi ili wananchi waweze kupata huduma iliyobora na yenye uhitaji mkubwa”. Amesema Mhe. Kigae

Aidha amewataka wananchi kutumia mataili yenye ubora ili kulinda usalama wa watu na siyo kuangalia mataili yenye gharama nafuu huku yakiwa hayana ubora unaotakiwa hivyo kusababisha ajali barabarani.

Naye, Mwenyekiti wa Kampuni ya ‘Superdoll’ bwana Seif Ali Seif amebainisha kwamba ushirikiano huu wa miaka 30 kati ya ‘Superdoll’ na ‘Michellin’ umeiwezesha Tanzania kutumia matairi bora ya kisasa ambayo ni salama zaidi kwa vyombo vya usafiri.

Hafla ya Maadhimisho hayo imehudhuriwa na Rais wa Michellin wakiwemo viongozi wengine wazito wa Kampuni hiyo, balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajlaoui , wateja wa kampuni ya ‘Superdoll’ na watu wengine mashuhuri hapa nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!