Home Kitaifa SERIKALI YAWEKA REKODI NYINGINE MPYA YA HUDUMA YA MAJI WANANCHI WATOA KONGOLE...

SERIKALI YAWEKA REKODI NYINGINE MPYA YA HUDUMA YA MAJI WANANCHI WATOA KONGOLE KWA MAMA SAMIA NA MBUNGE WAO ANNA KILANGO.

Na Dickson Mnzava, Same.

SHANGWE NDEREMO VYATAWALA KWA WANANCHI WA MROYO,KIZANGAZE KIJIJI CHA MPIRANI BAADA YA KUPATA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA.

Zaidi ya wananchi 5080 wa vitongoji vya mroyo na kizangaze katika Kijiji cha Mpirani kata ya Maore wilayani Same Mkoani Kilimanjaro wameweza kuondokana na adha ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwenye makazi yao.

Aidha wananchi hao wameipongeza serikali ya awamu ya sita kwakuweza kutegua kitendawili hicho ambacho kimedumu tokea Uhuru wa Tanganyika kwa wananchi hao ambao awali wamekuwa wakifuata huduma hiyo maeneo ya mbali zaidi na walikuwa wakitumia maji Kutoka kwenye bwawa la mifugo.

Wananchi hao wameipongeza Mbunge wa Jimbo la Same mashariki Anna kilango Malecela kwajuhudi zake na moyo wa dhati katika kuwapigania wananchi wake wakisema Mbunge huyo ni kiongozi wa kuigwa na viongozi wengine kwenye jamii katika kutetea maslahi mapana ya wananchi.

Wakizungumza katika kitongoji cha Mroyo mbele ya mbunge wao wananchi hao akiwemo Mariam Mussa na Rehema Ally wamesema wamekuwa wakipata adha ya upatikanaji wa huduma hiyo ya maji kitu ambacho kilikuwa kikihatarisha hata usalama wa ndoa zao.

Wamesema awali walikuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji kwaajili ya familia zao huku maji hayo walikuwa wakiyapata kwenye mabwawa ya mifugo na wakati mwingine kutumia muda mrefu kufuata huduma hiyo kitu ambacho kilipelekea hata wengine kuambulia vipigo Kutoka kwa waume zao.
“Kweli kabisa tunamshuru Mama Samia na mbunge wetu mheshimiwa Anna kilango Malecela na diwani wetu Rashidi hakika viongozi hawa wametupigania sana hadi kupata mradi huu haikuwa kazi rahisi na kiukweli mwanzoni wengi wetu hatukuamini kama maji leo tungeweza kuchota hapa lakini serikali ya mama Samia imetegua kitendawili hiki hakika kwetu ni furaha na sasa ndoa zetu zipo salama”
“Walisema wananchi hao”.

Diwani wa Kata hiyo ya Maore Rashidi Juma akizungumza kwenye ziara ya mheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo Anna kilango amesema zaidi ya wananchi 5080 wa Vitongoji vya Mroyo na Kizangaze watanufaika na mradi huo huku akiwataka wananchi hao kutunza miundombinu ya mradi huo ili uweze kuwanufaisha wao na kizazi kijacho.

Naye Mbunge wa Jimbo hilo mheshimiwa Anna kilango Malecela akiwa kwenye ziara yake kwenye kitongoji hicho amewatoa wasiwasi wananchi hao akisema serikali ikiahidi jambo kwa wananchi wake lazima itekeleze hivyo kuwasihi wananchi kuwa na amani na serikali yao na kuendelea kuwaamini viongozi wao waliowachagua kwani serikali ya Chama cha mapinduzi ipo imara katika kutetea maslahi mapana ya wananchi wake.

Mradi huo wa maji uliotekelezwa na wakala wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) utahudumia wananchi wapatao 5080 kwa vitongoji vya mroyo na kizangaze Kijiji cha Mpirani kata ya Maore na utahudumia wananchi wa kijiji cha Makokane Kata ya Kalemawe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!