Home Kitaifa SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAJASRIAMALI NA WAFANYABIADHARA KUWAWEZESHA KIUCHUMI

SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WAJASRIAMALI NA WAFANYABIADHARA KUWAWEZESHA KIUCHUMI

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema itahakikisha bajeti inayotengwa na kuelekezwa katika Halmashauri kuwawezesha Wafanyabiashara na Wajasrimali inawafikia moja kwa moja ili ikawasaidia kuinua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa kuongezeka.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said ikiwa ni mwendelezo wa siku ya pili ya Kongamano la Wanawake na Vijana katika biashara chini ya Eneo huru la Biashara Afrika linalofanyika kuanzia Swptemba 12 hadi 14 , 2022 JNICC Dar es Salaam

Vilevile amesema kwa Upande wa Zanzibar tayari zimetengwa fedha na kuwekwa katika benki ya CRDB ambayo inamuwezesha mwananchi kuchukua Mkopo pasipokuwa na riba wala kuweka dhamana kwani hapo awali wengi walikuwa wanakosa mikopo hiyo kwa kushindwa kupata vigezo hivyo vya dhamana

Serikali ya Zanzibari iliona adha ya wananchi wake kukosa mikopo hivyo Serikali imepunguza ule mzigo uliokuwepo wa riba kubwa na kuweka dhamana ili mtu apate mkopo na sasa kila mtu ananufaika na fursa hiyo uaminifu wa kirudisha na wengine wapate.

Sanjari na hayo amesema kwa Tanzania bara kulikuwepo na sheria mahusi na inayoziielekeza halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 Ili wananchi wakope wakajiendeleze katika shughuli zao za kiuchumi.

Aidha amesema kongamano hilo limekuwa chachu ya kubadilishana uzoefu, kujenga uhusiano wa kibiashara na kutatua changamoto za biashara hasa maeneo ya mipakani wanazokumbana nazo Wafanyabiashara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!