Na Neema Kandoro Mwanza
SHIRIKA LA Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) imetiliana saini na Kampuni ya Muhendislik Gemi Making Plas Ve Gd San Tic Ltd ya ujenzi wa Boti yenye vifaa vya matibabu kwa thamani ya sh bilioni 4.2.
Akizungumza katika utiaji saini Leo Jijini Mwanza Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile alisema mkataba huo ni wa miezi 12 ambapo boti itaweza kutoa suluhu kwa wananchi wa visiwani na mwambaoni mwa ziwa.
“Uwekezaji huu wa vifaa vya kisasa ndani ya ziwa utawezesha wananchi katika maeneo hayo kunufaika na huduma itakayotolewa” alisema Kihenzile.
Kihenzile alisema serikali kwa kuona kuwa watu waishio kwenye visiwa na pembezoni mwa ziwa wanakabiliana na changamoto za ukosefu wa boti ziwani kwa muda mrefu imeona uhitaji wa kuwezesha huduma hiyo ambayoi takuwa na uwezo wa kusafiri umbali wa kilomita 30 kwa saa moja.
Alisema Serikali ya Awamu ya sita imekuwa ikiwekeza fedha nyingi kwa usafiri wa majini na nchi kavu ili kuwezesha maeneo yote kupitika kwa urahisi na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi hapa nchini.