Na Shomari Binda-Musoma
SERIKALI imepingeza kasi na usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa mkoani Mara ikiwemo ya elimu,afya,maji na miundombinu.
Pongezi hizo zimetolewa leo oktoba mosi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora George Simbachawene katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku 4 mkoani Mara.
Akizungumza na watumishi kwenye ukumbi wa uwekezaji uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mara kabla ya kutembelea miradi iliyopo manispaa ya Musoma na Musoma vijijini amesema amesikia taarifa na kutambu kinachofanyika.
Amesema serikali imekuwa ikileta fedha nyingi mkoani Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na usimamizi mzuri uliopo wa fedha hizo kazi zinafanyika.
Simbachawene amesema ipo miradi ya shule mpya ambayo ililetewa fedha na imekamilika na wanafunzi wameingia madarasani na kupata elimu.
Amesema sio miradi ya elimu pekee bali kwenye sekta ya afy,maji na miundombinu imeletewa fedha na serikali na imefanyika vizuri.
” Nikushukuru sana mkuu wa mkoa chini ya uongozi wako na usimamizi mzuri kuhakikisha miradi inayoletewa fedha na serikali inasimamiwa vizuri.
” Sina mashaka na nguvu kazi ya mkoa wa Mara na inapaswa watumishi kufanya kazi kwa uadilifu na kujituma ili kuwaletea wananchi maendeleo”,amesema.
Amesema changamoto zilizoelezwa ikiwemo fidia kwa wananchi serikali itaendelea kuzifanyia kazi.
Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Evansi Mtambi ameishukuru serikali kwa kuendelea kuleta fedha nyingi mkoani Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Amesema mkoa umepokea zaidi ya milioni 500 kwaajili ya utekelezaji wa miradi na ipo iliyokamilika na mingine inaendelea kutekelezwa.
Akiwa Wilaya ya Musoma Waziri huyo ametebelea ametemelea shule ya sekondari ya wasichana Songe na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa majengo mapya ya madarasa kisha kufungua daraja la majengo na kisha kufungua hospital ya Wilaya iliyopo Suguti Musoma vijijini