Home Kitaifa SERIKALI YAONGEZA BAJETI YA MIKOPO ELIMU YA JUU

SERIKALI YAONGEZA BAJETI YA MIKOPO ELIMU YA JUU

Na. Magreth Mbinga

Serikali imeongeza bajeti ya mikopo ya elimu ya juu hadi kufikia shilingi 654 bilioni kutoka shilingi 570 bilioni za awali, sawa na ongezeko la asilimia 14.7 ambazo zinaenda kusaidia kwa kiasi kikubwa kwa wanafunzi ambao wapo vyuoni.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa elimu,sayansi na teknolojia Prof Adolf Mkenda katika mahafali ya kumi na tano ya Chuo Cha Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam.

Pia amesema wamekuwa wakitenga bajeti kwa ajili ya motisha kwa wahadhiri wa vyuo vikuu nchini wanaochapisha tafiti zao katika majarida makubwa duniani ili waweze kutambulika ulimwenguni kama watafiti wabobezi.

Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imetenga shilingi Bilioni moja, ambapo kila mtafiti atakayekidhi vigezo atapata shilingi milioni 50”. Amesema Prof.Mkenda.

Aidha Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Nchini Tanzania, Prof.Eliab Opiyo amesema Chuo kimejipanga kuanzisha masomo ya Shahada ya uzamili na uzamivu katika mwaka wa masomo 2022/2023 kwa kukamilisha uandishi wa mitaala inayokidhi mahitaji ya sasa na ya siku za mbeleni.

Hata hivyo amewataka wahitimu kutumia maarifa na ujuzi walioupata kuwatumikia Watanzania kwa nidhamu na uadilifu “Chukieni rushwa, zingatieni na kutii sheria, na tendeni haki”.

Amesema Chuo kimefanya juhudi mbalimbali kuzidi kuongeza ubora wa elimu inayotolewa chuoni ikiwemo kuendesha Chuo kufuatana na Mpango Mkakati wa Chuo wa miaka 5 (2021/22-2025/26) ambao unasisitiza kuandaa wahitimu mahiri na wenye ubunifu ili kuchangia katika kuifikisha Tanzania katika uchumi wa juu zaidi.

Sanjari na hayo Mjumbe wa bodi ya Chuo hiko Anosisye Mwakiposa amesema Chuo Cha Mtakatifu Joseph kinafundisha na kutoa wataalamu wa fani mbalimbali kama Wahandisi,Madaktari,Wauguzi na aina nyingine nyingi za fani.

Sisi kama bodi tumefurahi sana Wanafunzi kuhitimu ili wakaendelee na kazi na wengine wakjiendeleze ikiwa ni pamoja na kutangaza Chuo kwa uweledi ambao watauonyesha katika maeneo y kazi kwasababu Chuo Cha Mtakatifu Joseph mpaka sasa kimetoka wanafunzi wengi sana na wamefanya vizuri katika maeneo mbalimbali” amesema Mwakiposa.

Vilevile Mwakiposa amemelizia kwa kusema Chuo hiko kinamaadili kuanzia mvazi hadi tabia kwasababu ya muundo wa Chuo hiko toka kuanzishwa kwake kilizingatia swala hilo muhimu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!