Home Kitaifa SERIKALI YAMPONGEZA MBUNGE MATHAYO KUFANIKISHA MAFUNZO YA UDEREVA KWA WAENDESHA BODABODA NA...

SERIKALI YAMPONGEZA MBUNGE MATHAYO KUFANIKISHA MAFUNZO YA UDEREVA KWA WAENDESHA BODABODA NA BAJAJ

Na Shomari Binda-Musoma

SERIKALI imempongeza mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kufanikisha kupata mafunzo ya udereva kwa waendesha bodaboda na bajaj.

Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wa wilaya ya Musoma Dk.Khalfan Haule wakati wa kukabidhiwa vyeti kwa waendesha bodaboda na bajaj 220 waliohitimu mafunzo hayo chuo cha Veta Mara.

Amesema awali alimpa mbunge wazo la umuhimu wa waendesha bodaboda na bajaj hao kupata mafunzo ili waweze kupata leseni na kupunguza ajali za barabarani na kukubaliwa ombi lake.

Haule amesema mbunge amefanya jambo kubwa kwa kuwezesha kupatikana kwa mafunzo hayo na wale waiiyoyapata wamedai kunufaika na mafunzo hayo kwa kuwa kuna vitu vingi walikuwa hawavifahamu.

” Nikushukuru na kukupongeza mhwshimiwa mbunge kwanza kwa kukubali wazo na kulipokea na kuwezesha mafunzo ambayo yamewasaidia vijana wetu.

” Baada ya hapa watakwenda kupata leseni ambazo zitawawezesha kufanya kazi zao kwa uhuru na umakini na kuepuka ajali”amesema Haule.

Diwani wa Kata ya Mukendo Abasi Chamba kwa niaba ya Meya Patrick Gumbo na madiwani wa manispaa ya Musoma amemshukuru mbunge Mathayo kwa jambo jema alilolifanya kwa wasafirishaji hao.

Amesema ni vyema sasa wakaenda kuyatumia mafunzo hayo vizuri ili lengo la kupunguza na kumaliza ajali barabarani liweze kufanikiwa.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema mafunzo hayo sio mwisho yataendelea kutolewa kwa wale ambao hawajayapata.

Amesema kupitia ofisi ya bodaboda ambayo anaihudumia kwa kulipia kodi ya pango na muhudumu wa ofisi na ile ya bajaj waitumie kujisajili kwa wale ambao hawajapata mafunzo.

Mathayo amesema amekuwa mtetezi na mfatiliaji wa shughuli za bodaboda na sio wa jimbo la Musoma mjini bali nchi nzima ili waweze kufanya kazi zao na kutambuliwa kama kazi nyingine.

Kwa upande wao waendesha bodaboda hao na bajaj wamemshukuru mbunge Mathayo kwa fursa aliyowapa ya kupata mafunzo ya udereva Veta na kupata vyeti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!