Home Kitaifa SERIKALI YAJIVUNIA MFUMO WA KIDIJITARI WA MANUNUZI  YA UMMA (NeST) KUZIBA MIANYA...

SERIKALI YAJIVUNIA MFUMO WA KIDIJITARI WA MANUNUZI  YA UMMA (NeST) KUZIBA MIANYA YA RUSHWA

Na Lusungu Helela – Arusha 

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Ridhiwani Kikwete  anesema eneo la ununuzi wa umma limekuwa likiripotiwa kugubikwa na vitendo vya rushwa na ubadhirifu ambapo  zaidi ya asilimia 72 ya bajeti ya Serikali imekuwa ikitumika kwenye manunuzi  hayo ya umma 

Amesema kutokana na  uzito huo  Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao imeamua kusanifu, kujenga na kusanikisha Mfumo wa Kitaifa wa Kielektroniki wa Ununuzi Tanzania {National e-Procurement System of Tanzania (NeST)} ili kuweza kukabiliana na changamoto hiyo. 

Mhe.Kikwete ametoa kauli hiyo leo Jijini Arusha wakati akifunga  kongamano  la 14 la mwaka la wataalam wa ununuzi na ugavi zaidi ya 900 lenye kauli mbiu “Mabadiliko ya kidijitali kwa ajili ya kuboresha usimamizi na ugavi kelekea maendeleo endelevu

Amesema mfumo huo utasaidia  kuondoa mianya ya rushwa na upendeleo na hivyo thamani ya pesa za Serikali katika bidhaa na huduma italindwa kwani kutakuwa hakuna  ulazima wa  watu kukutana ana kwa ana

Ni furaha yangu mimi kama Naibu Waziri ninayeshughulikia Utawala Bora ambapo ninasimamia uzuiaji na mapambano dhidi ya Rushwa, naamini mfumo huu  utaondoa hisia hasi zilizojengeka katika jamii kwenye suala la manunuzi ya umma na hivyo kuongeza  uwazi ” amesema Mhe.Kikwete 

Mhe.Kikwete amesema u mfumo huo utaongeza ufanisi, uwazi na ushindani katika ununuzi wa umma. 

Katika hatua nyingine, Mhe.Kikwete amesema serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayesababisha upotevu wa rasilimali za nchi huku akiwataka wasithubutu kucheza na mfumo huo mpya wa manunuzi kwa umma.

Aidha, ametoa wito kwa waajiri wote kuhakikisha wataalam wenu wamesajiliwa na wanazo sifa za kufanya kazi za ununuzi na ugavi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi kupitia mfumo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!