Home Kitaifa SERIKALI YAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI

SERIKALI YAENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita itahakikisha inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza uchumi wa Nchi.

Amebainisha hayo alipokuwa anahutubia wakati akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Doto Biteko katika Kongamano la Biashara la Watendaji Wakuu 200, Agosti 29,2024, Dar es Salaam.

Dkt.Jafo amesema kama Serikali itaendelea kuunga mkono sekta binasfi na kufanya sekta ya uwekezaji na biashara Nchini kuwa sekta zinazofanya vizuri ndani na nje ya Tanzania na ndio maana mpaka sasa inaendelea kufanya mapinduzi katika kuweka upya mifumo ya biashara Pamoja na kujenga miundombinu ya usafirishaji itakayosaidia mazingira wezeshi ikiwemo ujenzi wa barabara,Reli ya kisasa ya mwendokasi,ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere Pamoja na mradi wa umeme vijijini.

Aidha Dkt.Jafo amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa Sekta binafsi kwani imekuwa mstari wa mbele katika kutoa ajira kwa vijana nchini kwani imekuwa moja ya sehemu inayopunguza presha kubwa ya ukosefu wa ajira nchini.

Vilevile Waziri Jafo ametoa rai kwa taasisi shiriki katika kongamano hilo kuchangamkia fursa mbalimbali za masoko ambazo Serikali imeweza kupata kiwemo masoko ya kikanda kama vile SADC, AGOA,Soko la Ulaya na soko la Afrika Mashariki ili kuongeza maendeleo ya sekta ya biashara nchini.

Kongamano hilo ni moja ya kongamano linalowakutanisha kwa pamoja Watendaji Wakuu wa makampuni na taasisi 200, Serikali na sekta mbalimbali kujadili mambo mbalimbali yatakayopelekea maendeleo mbalimbali ya viwanda na uchumi wa Nchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!