Home Kitaifa SERIKALI YAELEZA BAADHI YA MIKAKATI KUZUIA MDONDOKO WA WANAFUNZI

SERIKALI YAELEZA BAADHI YA MIKAKATI KUZUIA MDONDOKO WA WANAFUNZI

Akijibu swali la Mbunge wa Viti maaluum Bungeni Mhe. Hawa Mchafu Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Tenolojia Mhe. Omari Kipanga amesema mikakati ya Serikali ni kujenga shule za wasichana katika kila Mkoa ambapo tayari ujenzi wa shule 10 umeanza.

Ametaja mikakati mingine kuwa ni Ujenzi wa hostel katika maeneo yenye umuhimu wa kujengewa na kuanzisha vitengo vya elimu ya unasihi na ushauri kwenye shule.

Pia amesema Serikali itachukua hatua kali kwa wale wote waliothibitika kujihusisha kunyanyasa wanafunzi na kukatisha masomo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!