Home Kitaifa SERIKALI YAELEKEZA MILIONI 573 UJENZI WA WANYERE SEKONDARI

SERIKALI YAELEKEZA MILIONI 573 UJENZI WA WANYERE SEKONDARI

Na Shomari Binda-Musoma

SERIKALI kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024 ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI) itatoa kiasi cha shilingi milioni 573 kupitia mradi wake wa SEQUIP kwa ajili ya ujenzi wa sekondari mpya kijijini Wanyere.

Hii itakuwa ni sekondari ya pili ya Kata ya Suguti kujengwa ili kuwapunguzia umbali mrefu wanafunzi kwenda kupata elimu.

Wananchi wa kijiji cha Wanyere wameanza kuchangia nguvu kazi za kusomba mchanga, mawe, maji na kuchimba msingi wa jengo moja la madarasa 2 na ofisi 1 ya walimu.

Ili kuunga mkuno juhudi za wananchi hao na serikali,mbunge wa jimbo la Musoma vijijini, Prof. Sospeter Muhongo,ameanza kwa kuchangia mifuko 100 ya saruji kwenye harambee iliyofanyika kijijini Wanyere.

Licha ya kuendesha harambee ya kuanza ujenzi huo, alitembelea Kijiji cha Wanyere kwa malengo makuu mawili ikiwa ni kusikiliza kero za wanakijiji na kuzitatua na kuhamasisha ujenzi wa sekondari mpya kijiji hapo.

Katika harambee hiyo, wananchi wa Kijiji jirani cha Kataryo wamechangia saruji mifuko 30 na kiasi cha shilingi milioni 2.5 zilichangwa ili kuunga mkono juhudi hizo za kuinua elimu.

Mimi wananchi wakiwa tayari kwenye suala la maendeleo yakiwemo ya elimu nipo tayari kuchangia na kwa kuanzia ntatoa mifuko 100 ya saruji”,amesema Muhongo.

Wakati jitihada hizo zikiendelea bado halmashauri ya wilaya ya Musoma haijatoa mchango wowote katika kufanikisha ujenzi wa shule hiyo.

Wananchi na viongozi wa jmbo la Musoma Vijijini wanaishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuongeza ubora wa utoaji wa elimu jimboni kwao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!