Home Kitaifa SERIKALI: USHIRIKIANO MZURI NA JAPANI UMELETA TIJA UWEKEZAJI KATIKA MIUNDOMBINU

SERIKALI: USHIRIKIANO MZURI NA JAPANI UMELETA TIJA UWEKEZAJI KATIKA MIUNDOMBINU

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia wizara ya Uchukuzi imesema itaendelea kujenga mashirikiao mazuri na Serikali ya Japani ili waendelee kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ikiwemo miradi barabara reli bandari ili kusaidia kujenga mazingira wezeshi kwa wafanyabishara wanasafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii, kutoka Japan Konosuke Kokuba pamoja na wawekezaji mbalimbali kutoka nchini humo kujadili fursa mbalimbali za uwekezaji hapa nchini ambapo amesema kuwa Tanzania wameshuhudia Miradi iliyojengwa na Japani ikiwemo Daraja la Salenda na Daraja la Mfugale ambalo Serikali ilijenga kwa msaada na li
limedumu mpaka leo yamekuwa yakitumiwa bila dosari yeyote.

“Ukweli fursa tunazoziona kwa wawekezaji katika nchi zilizoeendelea ikiwemo nchi ya Japani Mfano Daraja la.Salenda limejengwa mda mrefu sana na ni la kudumu halina dosari yeyote tunakubali wenzetu hawa ni wazuri sana pia wametujengea flyover daraja la Mfugale kwa msaada bure na hawatudai chochote” amesema Waziri

Waziri Prof. Mbarawa amewasisitiza wawekezaji katika sekta ya uchukuzi kutoka Japan kuja kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati ikiwemo maeneo ya bandari na reli ambayo yana tija kwa pande zote.

Hata hivyo ametaja maeneo yanayohitaji uwekezaji kuwa ni pamoja TPA ujenzi wa kituo cha kuhifadhi makasha katika bandari ya Dar es Salaam, ujenzi wa barabara ya reli ya Isaka-Lusumo-Kigali yenye urefu wa kilomita 495.

Sambamba na hayo amesema sababu zilizopelekea kuongeza kwa Meli Tanzania ni pamoja na uwezeshaji toka serikalini, ongezeko la kina cha lango la Bandari hadi mita 15.5 ambacho kinatosha kuhudumia Meli gatini.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Reli TRC Mhandisi Masanja Kadogosa amesema serikali kupitia TRC inawajibu wa kujenga miundombinu ya reli inayovutia waekezaji kuitumia hivyo suala la sheria kwamba reli ijengwe na kuruhusu wawekezaji Watanzania na watu kutoka nje ya nchi kuwa na treni zao kuziendesha kubeba abiria na mizigo kutoka sehemu moja kwenda nyingine hii ni fursa pekee iliyopo Tanzania .

Reli yetu ina uwezo wa kubeba tani milioni 17 ha milioni 25 huu ni uwekezaji kwani muwekezaji anaweza anafanya tani 6 hadi 10 kwani serikali haifanyi biashara kazi yake ni kutengeneza mazingira yanayoruhusu Wananchi na wawekezaji kutoka nje ya nchi kufanya biashara.

Kadogosa amesema kuna dhana imejengwa kwamba Reli inashindana na Malori amekanusha kuwa ni dhana isiyo na maana kwani reli inaleta neema kwa watu wenye malori kupunguziwa kutembea na mizigo umbali mrefu kwa kutumia treni wao watakuwa wanasafirisha mizigo sehemu ambapo miundominu ya treni haijafika .

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Bandari TPA Plasduce Mbossa amesema Bandari ya Dar es salaam katika kipindi cha miaka kadhaa imekuwa ikiendelea kupokea Meli kubwa za mizigo na kuna Magati 12 hivyo tayari kuna Magati yamepata muwekezaji na tutarajie makubwa kwani Tanzania imezungukwa na nchi 7 ambazo hazina bandari hivyo hutumia bandari ya Dar es salaam hivyo ni fursa kibiashara.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Usafiri na Utalii kutoka Serikali ya Japan, Mhe. Konosuke Kokuba, amesema kuwa wataendelea kuimarisha mahusiano kati ya nchi hizo kwa kuendelea kujenga miundombinu yenye ubora katika miradi yote inayoendelea na ile ambayo inatarajiwa kutekelezwa.

Amesema kuwa kutokana ongezeko la watu katika nchi zinazokuwa zinahitaji teknolojia za kisasa katika ujenzi wa miundombinu nchini ili ziweze kutosheleza mahitaji.

Haya yanajiri ikiwa ni siku chache tu zilizopita ambapo Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa alitembelea Bandari ya Dar es Salaam kuendeleza uhusiano wa kibiashara baina ya nchi yake na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania – TPA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!