Home Kitaifa SERIKALI KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA KUBORESHA TAASISI ZA HAKI JINAI NCHINI

SERIKALI KUYAFANYIA KAZI MAPENDEKEZO YA KUBORESHA TAASISI ZA HAKI JINAI NCHINI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali zote mbili zitafanyia kazi mapendekezo yaliyowasilishwa Serikalini kuhusu kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za haki jinai nchini ili kutoa huduma na kuleta mageuzi pamoja na kutekelezeka kwa ufanisi zaidi katika mifumo ya utoaji wa haki nchini.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 09 Septemba 2023 akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha Taasisi za haki jinai, Jaji Mkuu Mstaafu Mhe. Mohamed Chande Othman akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Balozi Ombeni Yohana Sefue na ujumbe wao waliofika Ikulu, Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar inapata ushirikiano wa karibu na msaada wa kujengewa uwezo kutoka Taasisi za Tanzania Bara ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi Zanzibar (ZAECA) pia ushirikiano kati ya Mamlaka ya kudhibiti na kuzuia dawa za kulevya Zanzibar na DCEA katika kufanya kazi kwa pamoja kuvidhibiti vitendo hivyo ambavyo vinahusisha mipaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!