Na Shomari Binda
SERIKALI imeahidi kukaa na kuzungumza na mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete ili kuzungumzia ujenzi wa kilometa 5 za ujenzi wa barabara wilayani Tarime.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Tamisemi Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge huyo.
Amesema serikali inatambua umuhimu wa barabara hiyo hivyo watakaa na mbunge Ghati ili kuona namna ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Mheshimiwa Spika tutakaa na mbunge na kuzungumza nae kuona namna ya ujenzi wa kilometa 5 ya barabara hii wilayani Tarime”, amesema.
Katika kikao cha 9 cha mkutano wa 13 wa bunge la 12 linaliendelea kwenye kipindi cha maswali na majibu mheshimiwa Ghati Chomete aliuliza ni lini serikali itaanza ujenzi wa barabara wa kilometa 5.
Akizungumza na Mzawa Blog baada ya kipindi cha maswali na majibu,mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete amesema wilaya ha Tarime inazalisha mazao mbalimbali hivyo inahitaji barabara zinazopitika.
Amesema kilometa 5 ambazo ameziulizia iwapo ujenzi wake utajengwa utasaidia katika usafirishaji wa mazao ya wakulima .
Mbunge Ghati amesema anaamini wakikutana na kukaa na serikali watazungumza na kufikia hatua ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Nashukuru serikali sikivu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na majibu yaliyotolewa na Naibu Waziri na barabara hii itakwenda kujengwa” amesema Ghati.