Home Kitaifa SERIKALI KUIMARISHA TEHAMA, KUFUTA TOZO ILI KUJENGA UCHUMI FUNGAMANI

SERIKALI KUIMARISHA TEHAMA, KUFUTA TOZO ILI KUJENGA UCHUMI FUNGAMANI

Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka Mazingira Wezeshi kwa Uendeshaji wa Biashara na Uwekezaji kwa kuimarisha mifumo ya TEHAMA, kufuta au kupunguza tozo, ada na fine ili kujenga Uchumi wa Viwanda unaofungamanisha Uchumi na Maendeleo ya Watu.

Aidha, Serikali inachukua hatua mbambali zinazolenga kutekeleza miradi ya kimkakati ambayo itakuwa na matokeo makubwa katika Sekta ya Viwanda na nyingine za kiuchumi katika nchi yetu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb.) Oktoba 10, 2022 wakati akifunga Maonesho ya tatu ya Wiki ya Biashara na Uwekezaji Mkoani Pwani yaliyofanyika Mailmoja, Kibaha kuanzia tarehe 05 hadi 10, Oktoba 2022.

Aidha, Kigahe ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika Mkoa wa Pwani maana kuna Ardhi ya kutosha na fursa mbalimbali ambapo hadi sasa Mkoa huo una Viwanda 1,460, na kati ya hivyo Viwanda 90 ni Viwanda Vikubwa.

Hivyo, nitumie fursa hii kuendelea kuwahimiza Wawekezaji wa ndani na nje kuchangamkia fursa hii. Waje wawekeze Mkoa wa Pwani kuna fursa mbalimbali, Ardhi ya Kutosha na Miundombinu rafiki kwa Uwekezaji ikiwemo Umeme, Maji, Barabara na Ulinzi na Usalama.” Amesema Kigahe.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amesema anaruhusu wawekezaji kuwekeza katika ardhi kwa lengo la kujenga viwanda. Kupitia uwekezaji huo unasaidia kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja,kuongeza wigo wa mapato ya serikali kupitia Kodi na tozo nafuu.

Aidha amesema kutokana na kuboreshwa kwa miundombinu muhimu ya Uwekezaji , Uwepo wa Viwanda nchini unaendelea kutoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, lakini pia viwanda hivi vinaongeza kuchochea ukuaji wa Sekta mbalimbali kama vile Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Usafirishaji na Teknolojia. Aidha, vinaendelea kuongeza wigo wa Mapato ya Serikali kupitia kodi na tozo nafuu na rafiki za ushuru mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!