Home Kitaifa SERIKALI KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KUPUNGUZA GHARAMA ZA BEI ZA VYAKULA

SERIKALI KUCHUKUA HATUA MADHUBUTI KUPUNGUZA GHARAMA ZA BEI ZA VYAKULA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Husein Ali Mwinyi amesema Serikali ya awamu ya nane itaendelea kuweka jitihada za kupunguza gharama za bidhaa za vyakula katika kipindi cha kuelekea mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Ameyasema hayo leo baada ya sala ya Ijumaa msikiti wa Forodhani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi.

Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuweka mipango madhubuti itakayowezesha kupunguza gharama za bei za vyakula.

Katika Ibada hiyo ya ijumaa Rais Dk.Mwinyi amehahidi kuchangia sh.milioni tano kukarabati msikiti huo wa Forodhani.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!