Home Kitaifa SERIKALI ITAENDELEA KUWASILISHA TAARIFA KUHUSU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

SERIKALI ITAENDELEA KUWASILISHA TAARIFA KUHUSU UTATUZI WA CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu maswali kuhusu utatuzi wa changamoto za Muungano bungeni jijini Dodoma leo Novemba 8, 2023.

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imesema itaendelea kuwasilisha taarifa kuhusu utatuzi wa changamoto za Muungano unaofanyika kupitia vikao baina ya Serikali zote mbili.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Asya Mwadini Mohammed aliyetaka kujua kama kama Serikali haioni haja ya kuwasilisha bungeni taarifa za mchakato mzima wa utatuzi wa changamoto za Muungano.

Akijibu swali hili Waziri Jafo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa ikiwasilisha taarifa hiyo katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ambayo inaisimamia.

Amesema kuwa hivi karibuni katika vikao vya Kamati za Bunge, miongoni mwa taarifa zilizowasilishwa ni pamoja na ile inayozungumzia Changamoto za Muungano zilizotatuliwa na zile ambazo zinaendelea kutatualiwa ili wananchi wapate ufahamu wa kazi hiyo kubwa inayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).

“Nimpongeze mbunge kwa swali lake zuri na tunaahidi kuwa tutaendelea kuleta taarifa za kila tunapotatua changamoto hizi za Muungano katika Bunge lako tukufu Mheshimiwa Naibu Spika hususan katika kipindi cha bajeti na tutaendelea kufanya hivyo kwa vikao vijavyo,“ amesisitiza Dkt. Jafo.

Awali Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mohamed Said Issa aliyetaka kujua mafanikio baada ya utatuzi wa changamoto za Muungano, ameyata kuwa ni ya kiuchumi, kijamii na kisiasa hasa katika maeneo ajira kwa Watumishi wa Zanzibar wanaofanya kazi katika Taasisi za Muungano, wameendelea kunufaika na ajira hizo ikiwa ni asilimia 79 kwa Tanzania bara na 21 kwa Zanzibar.

Pia, Mgawanyo wa Fedha za Mapato yatokanayo na Misaada na Mikopo  Nafuu ya Kibajeti (GBS) imeendelea kuongezeka tangu kupatiwa ufumbuzi wa kero hii na  kuendelea kuimarisha  Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa  pande zote mbili za Muungano.

Naibu Waziri Khamis amesema tangu kuasisiwa kwa Muungano Serikali zliona haja ya kuunda kamati ya kutatua changamoto katika ngazi mbalimbali.

Ameongeza kwa kusema kuwa kamati hiyo inafanya vizuri ndio maana yamepatikana mafanikio makubwa katika utatuzi wa changamoto za Muungano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!