
Na Magrethy Katengu – Dar es salaam
Serikali itaendelea na jitihada za kuhakikisha inajenga vituo vingi vya afya na kuboresha miundombinu ikiwemo vifaa tiba na usafiri ili kusaidia kila mtu anapohitaji huduma ya afya ahudumiwe vizuri na watoa huduma.
hayo yamesemwa leo Mei 17, na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo katika hafla ya ugawaji bajaji 18 na vibao vya kupima Urefu watoto walio chini ya umri wa miaka mitano, vifaa hivuo ni kwa ajili ya kusaidia upatikanaji wa huduma na kutekeleza afua za lishe.

Aidha Mpogolo amesema vipimo hivi vitakwenda kusaidia kujua uzito wa mtoto kuanzia anapozaliwa kama anauzito unaostahili ili aweze kusaidiwa kwenye eneo hilo, hivyo fedha zilizotengwa ni zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zinaenda kwenye afua za lishe na miongoni mwa fedha hizo milioni 22 zimekwenda kununua vipimo hivi kwa ajili ya watoto.
Hata hivyo Mpogolo amesema kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM imeahidi kuboresha huduma za Afya na moja ya maboresho ni eneo la ujenzi wa miundombinu ambapo Mhe Rais Dkt Samia ametenga zaidi ya Dolla bilioni 26 kuboresha miundombinu katika halmashauri ya jiji la Ilala na ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vikubwa viwili vya afya, Mchikichini kinachogharimu kiasi cha fedha bilion 5 na kituo cha Mzinga mradi wenye thamani ya bilioni 2.5 na na hadi sasa kuna vituo vya afya zaidi ya 10 na vipo katika hatua za mwisho kukamilika .

Naye Mganga Mkuu Halmashauri ya Jiji la Ilala Dkt Zaituni Hamza amesema moja ya shuguli zao ni kutekeleza vipaumbele muhimu vya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, katika fedha walizotengewa wamenunua vifaa zikiwemo bajaji za kufutilia makuzi ya mtoto nyumba kwa nyumba , chanjo, lishe, shughuli za kutokomeza Malaria Nchini na ustawi wa jamii
Aidha watumishi wote waliokabidhiwa vifaa hivyo wameombwa kuvitunza vizuri na kuvitumia kwa mlengo uliokusudiwa.