Mbioni kufungua soko la pamoja la wafanyabiashara wa Madini Mererani
Na.Samwel Mtuwa – Arusha.
Serikali kupitia Wizara ya Madini imewahakikishia wafanyabiashara ya Madini mkoani Arusha kuwa ipo tayari kutatua changamoto zote zinazowakabili wafanyabiashara wa madini mkoani humo.
Hayo yamebainishwa leo Desemba 22,2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali wakati wa ziara ya kikazi mkoani Arusha alipotembelea masoko ya madini katika eneo la Uzunguni.
Akizungumza na wafanyabiashara hao mapema baada ya kupokea taarifa ya mwenendo wa biashara ya madini mkoani Arusha kutoka kwa mwenyekiti wa soko la madini Abost Mollel, Katibu Mkuu Kheri Mahimbali amefafanua kuwa Serikali inatambua kuhusu changamoto hizo na ipo katika hatua mwisho za utatuzi ambapi hivi karibuni tamko litatolewa.
Kwa upande wake, Mweyekiti wa Wafanyabiashara soko la madini Arusha Abogast Mollel amesema kuwa kwasasa biashara ya madini imekuwa ngumu kutokana na soko la madini kuamishiwa Mirerani jambo ambalo limesababishia wafanyabiashara wengi wa madini ya Tanzanite kufunga biashara zao.
Akielezea kuhusu mwingiliano wa biashara katika soko moja Mollel amesema kwamba kwasasa tunashindwa kupata takwimu sahihi za mauzo na manunuzi ya madini kutokana na mwingiliano wa wafanyabiashara na wanunuzi kuwa katika eneo moja jambo linalopelekea kutokupatikana kwa usahihi wa taarifa.
Naye mwenyekiti , wa wafanyabiashara wa madini ya vito Tanzania Osman Tharia ameishukuru Serikali kwa kufanya ziara katika eneo la soko kwasababu anaamini kwa kufanya hivyo kutatoa picha halisi ya hali inayoendelea katika masoko hayo na kupata njia sahihi za kuweza kutatua changamoto hiz.
Akielezea kuhusu leseni moja kutumika eneo hilohilo Thaira ameiomba Serikali kubadilisha mfumo kwani kuwa na leseni isiyovuka mipaka ni kuwafungia fursa katika maeneo mengine yenye fursa kama hizo.
Awali, Katibu Mkuu amekiembelea Kituo cha Jimolojia (TGC) Kinachotoa mafunzo ya kuongeza thamani madini ambapo aliweza kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo Maabara ya madini Vito,sehemu mpya ya ujenzi wa chuo , pamoja na kuongea na menejimenti ya Chuo.