Home Kitaifa Serikali imewahakikishia wawekezaji wote nchini kutumia fursa ya mazingira bora ya ufanyaji...

Serikali imewahakikishia wawekezaji wote nchini kutumia fursa ya mazingira bora ya ufanyaji biashara

Waziri wa Viwanda ana Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amewakikishia wawekezaji wote nchini kutumia fursa ya mazingira mazuri ya ufanyaji biashara yaliyowekwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais mhe. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipotembelea kongani ya viwanda ya kwala iliyopo katika wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani yenye ukubwa wa ekari 2500 mradi unaogharimu dola za kimarekani takribani milioni 327 na kongani hii itakapokamilika itaajiri watanzania zaidi ya laki moja.

Dkt. Kijaji amemtaka mwekezaji wa kampuni ya Sino Tan kuharakisha ukamilishwaji wa viwanda viwili vya awali ambavyo ni kiwanda cha mafuta ya kupaka na vipodozi pamoja na kiwanda cha nguo ambavyo vitakamilika ifikapo mwezi Oktoba 2023.

Naye mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Nicson John amesema kuwa mradi huo wa Sino Tan ukikamilika utachukua viwanda zaidi ya 250 na kutoa ajira zaidi ya laki moja na kwa awamu ya kwanza ya mradi huu ambao ni ujenzi wa viwanda viwili ukikamilika utaajiri watanzania zaidi ya mia tano (500).

Kwa upande wake Mwakilishi wa wa Sino Tan Kibaha Bw. Jensen Huang amesema kuwa mradi huo unaenda kutoa ajira za moja kwa moja zaidi ya 100,000 ambapo utapelekea kukua kwa uchumi wa nchi na mwananchi mmoja mmoja hasa wanaozunguka eneo la kiwanda.

Aidha Dkt. Kijaji ametembelea kiwanda cha kutengeneza maji tiba cha Kairuki pharmaceuticals limited na kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo kwa kushirikiana na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara na kushughulikia kwa haraka.

Meneja wa kiwanda cha madawa cha Kairuki Bi. Hellen Magita amesema kuwa ujenzi wa kiwanda ulikamilika desemba 2021 na kuanza uzalishaji, mpaka sasa wamesajili dawa 18 kwenye mamlaka ya dawa Tanzania (MSD) na kusajili katika nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo Malawi, Zambia, Kenya, Msumbiji na uwezo wa uzalishaji wa kiwanda ni chupa milioni 60 kwa mwaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!