Home Kitaifa SERIKALI IMETATUA CHANGAMOTO ZA UBIA NA TAASISI ZA DINI – BASHUNGWA

SERIKALI IMETATUA CHANGAMOTO ZA UBIA NA TAASISI ZA DINI – BASHUNGWA

Eliud Rwechungura – OR TAMISEMI

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeimarisha Ushirikiano na Taasisi na Mashirika ya kidini zinazotoa huduma ya Afya msingi kwa wananchi kwa kutatua changamoto zilizokuwepo baina ya taasisi za dini na Serikali.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa leo tarehe 02 Oktoba 2022 katika Maadhimisho ya miaka 125 ya Uinjilishaji Jimbo la Rurenge Ngara yaliyofanyika katika Kituo cha hija Katoke Biharamulo, Kagera.

Bashungwa amesema Serikali imefikia makubalinao na Taasisi za dini kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023 mgao wa fedha za Mfuko wa Afya katika Halmashauri zenye Hospitali ya Wilaya zitapokea asilimia 60 ya mgao na Hospitali Teule za dini za Wilaya zitapokea asilimia 40 ya mgao.

Serikali imefikia hatua hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa katika Jubilei ya Miaka 25 ya Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi iliyifanyika Februari 22, 2022 ya kuhakikisha Serikali inapitia upya makubaliano yaliyopo na taasisi za dini.

Bashungwa amesema kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itaandaa kanuni ya ugawaji wa fedha hizo utakaozingatia mzigo na uzito wa huduma katika hospitali husika na kanuni hiyo itaanza kutumika katika maandalizi ya bajeti ya Mwaka ujao.

Aidha, Bashungwa amesema fedha za Mfuko wa Afya wa Pamoja zinazotengwa kwa ajili ya Hospitali za Mashirika ya Dini zitatumwa moja kwa moja kutoka HAZINA kwenda kwenye akaunti za benki za Vituo husika zitakazofunguliwa kwa mujibu wa taratibu za Serikali ili kuondoa changamoto zilizopo.

Vilevile, amezitaka Halmashauri ziendelee kuingia mikataba ya ushirikiano na Hospitali teule za Halmashauri pamoja na Hospitali nyingine za Mashirika ya Dini zilizopo kwenye maeneo yao kulingana na mahitaji ya maeneo husika.

Kwa upende wake, Mhashamu Askofu Severine Niwemugizi wa Jimbo kuu la Ngara ameishukuru Serikali kwa kufanyia kazi Changamoto chote alizowasilisha kwa Mheshimiwa Rais na ahaikakikishia Serikali kuwa Viongozi wa Dini wataendelea kuunga Mkono kazi zote zinazofanywa na Serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!