Home Afya SERIKALI IMESHAURIWA KUTUNGA SHERIA YA AFYA YA UZAZI ITAKAYOWASAIDIA WANAWAKE.

SERIKALI IMESHAURIWA KUTUNGA SHERIA YA AFYA YA UZAZI ITAKAYOWASAIDIA WANAWAKE.

Na Mariam Muhando – Dar es salaam.

Serikali kupitia Wadau wa Masuala ya Afya ya Uzazi imeshauriwa kuweka mpango mkakati wa kutunga Sheria ya Afya hio ili iwezekumlinda Mwanamke katika kujifungua na kumkinga na maambukizi mbalimbali.

Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama Cha Wanasheria Wanawake TAULA Tike Mwambipile kwenye kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani ambapo Shirika linalojishughulisha na Masuala ya Afya Marie Stopes Tanzania imewakutanisha Wadau hao Jijini Dar es salaam Kwa lengo la kujadiliana masuala yanayomuhusu Mwanamke na Jamii Kwa Ujumla .

Mwapipile amesema katika kuadhimisha siku hiyo wameweza kujadili changamoto mbalimbali za masuala yanayohusu Afya ya Uzazi ambapo Marie stops inajitahidi kuhakikisha masuala ya Afya ya Uzazi yanapewa kipaumbele hivyo,”Wadau wauunge mkono juhudi hizo ili waweze kufikia lengo la jamii kuwa na uelewa kuhusu Afya ya Uzazi” alisema Mwapipile.

Amesema siku hio ni muhimu Kwa Wanawake kukutana ili kujadili mambo balimbali ambapo wao wamejadili masuala ya Afya ya Uzazi hivyo kauli mbiu yake ni Wekeza Kwa Wanawake kuhakikisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii ambapo kauli hio ni Moja ya majukumu katika kuangalia Afya ya hio hivyo eneo hilo linamuadhiri Mwanmke na jamii Kwa ujumla.

Nae Mkurugenzi wa huduma za Afya Marie Stopes Nchini Dr Jophrey Sigala amesema maadhimisho hayo yamejikita katika usawa na huduma za Afya ambapo wameangalia mambo mbalimbali ikiwemo kuangalia mafanikio ya Wanawake kwenye kufikiwa na huduma za Afya,”Tunaenda kuhakikisha Wakina mama Wengine ambao hawajafikiwa na huduma hi ili waweze kufikiwa” alisema Dr Sigala .

Sigala mesema bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo elimu bado haijaweza kuwafikia Watanzania wanaoishi Vijijini, hivyo baadhi ya Wanaume hawashirikishwi hivyo ni muhimu Kwa Wanaume kutambua elimu ya Afya ya Uzazi, huduma kuwafikia watu wote sawa na Watu wenye mahitaji maalum.

Akifafanua zaidi amesema takwimu zimeonesha nusu ya Wanawake bado hawajapata huduma za Afya ya Uzazi Kwa maamuzi yao hivyo watahakikisha wanatoa elimu kwa Jamii ili Watu waweze kuamua katika kufanya maamuzi yalio sahihi kwa kupata huduma hio na kupata taarifa sahihi kumewezesha jinsi ya kukabiliana na changamoto anazozipata za Uzazi.

Amesema Jamii inayowajibu wa kupata taarifa sahihi na uelewa Masuala ya Afya ya Uzazi Kwa kutumia miongozo ili kuyafikia makundi maaluum.

Aidha Marie stopes Tanzania imeweza kuwakutanisha Wadau mbalimbali waliojikita katika usawa na Masuala ya Afya ikiwemo Shirika linaloangalia Haki TAULA Shirika linalo angalia mipango mbalimbali ili kuhakikisha zinawafikia huduma DANIDA, watoa huduma ngazi ya jamii na Walenavu waliopata huduma ya Afya ya Uzazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!