Home Kitaifa #SensaBika: MASTAA WA SOKA, MUZIKI, FILAMU KUMUUNGA MKONO MAMA SAMIA NA SENSA

#SensaBika: MASTAA WA SOKA, MUZIKI, FILAMU KUMUUNGA MKONO MAMA SAMIA NA SENSA

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amezindia Programu Kabambe ya Wizara hiyo kutumia wadau wake wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi.

Kwakutambua juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan kuhamasisha sensa ili kuweka mipango mizuri ya maendeleo ni vyema sisi nasi sekta zetu zikaungana; kampeni hii itahusisha mastaa wote wa muziki, filamu na michezo kusambaza ujumbe wa sensa kisha Agosti 21 tutakuwa na Tamasha kubwa la michezo na sanaa,” alisema Waziri Mchengerwa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, ameielezea kampeni hiyo kuwa ni ubunifu mwingine wa Wizara hiyo katika kuchangia maendeleo ya Taifa akiwataka wadau wote kujitoa katika kuunga mkono kampeni hiyo.

Hii ndio wizara yenye watu ambao ni mahiri, wabobezi na watopezi wa kuhamasisha mambo mbalimbali ya kijamii; kampeni hii inawaleta pamoja wadau kutoa mchango wetu kwa kuhamasisha sensa,” alisema Dkt. Abbasi.

Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 20, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa Tanzania wanaokwenda kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!