DC Nyangasa awataka wananchi kutoa taarifa za wanaowahisi zifanyiwe uchunguzi , atoa namba maalum
-Awatahadharisha vijana kutojihusisha na vikundi vya uhalifu
- Ahimiza ulinzi shirikishi
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Fatma Almas Nyangasa amewaelekeza wenyeviti wa serikali za mitaa ambao pia ni wenyeviti wa kamati za ulinzi katika mitaa yao kuhakikisha ulinzi shirikishi unafanyika kikamilifu sambamba na utoaji taarifa ya hali ya usalama katika maeneo yao.
Aidha , DC Nyangasa amewataka wananchi kutoa taarifa haraka kwa jeshi la polisi juu ya mtu, kikundi au mazingira yoyote yenye mashaka ili zifanyiwe kazi kukabiliana na vitendo vya uhalifu kwa ujumla.
Katika kikao kazi Maalum na wenyeviti wa serikali za mitaa leo , DC Nyangasa amewatahadharisha vijana kutojihusisha na vitendo vya uhalifu na kwamba tayari
Jeshi la polisi Wilaya ya Kigamboni limeanza oparesheni Maalum kata kwa kata wilayani humo huku likitahadharisha vijana na kuwataka wazazi kuwaonya vijana wao.
Naye Mkuu wa Polisi wilaya ya Kigamboni OCD Walelo amesema timu yake iko timamu kuhakikisha usalama kigamboni unaendelea kuimarika, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano katika upatikanaji taarifa za wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.